http://www.swahilihub.com/image/view/-/4759280/medRes/2109634/-/15scuakz/-/kibajaji.jpg

 

Kibajaji ampaisha Waitara Ukonga

Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde maarufu kama ‘Kibajaji’ akiwataka wakazi wa Viwege Jimbo la Ukonga kumchagua Mwita Waitara  

Na Peter Elius

Imepakiwa - Friday, September 14  2018 at  13:59

Kwa Muhtasari

Atahakikisha serikali inafikisha umeme wa REA kwa bei nafuu ya Sh27,000 pekee

 

Dar es Salaam. Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde maarufu kama ‘Kibajaji’, amewataka wakazi wa Viwege Jimbo la Ukonga kumchagua mbunge ambaye chama chake kinafanya kazi.

Alisema kwa kumchagua Mwita Waitara jimbo hilo litakuwa na maendeleo kwani atakuwa karibu na Serikali hivyo matatizo yao yatatatuliwa haraka.

“Nitaungana naye bungeni kuitaka Serikali ifikishe umeme wa bei nafuu kupitia REA ili wananchi waunganishiwe kwa gharama ya Sh27,000 pekee.

“Mgombea pekee atakayemfurahisha Rais Magufuli ni Mwita Waitara. Kwanza anaingia dirisha dogo, mwakani tuna uchaguzi wa Serikali za mitaa lazima tufanye jambo hapa ili tupate cha kusema kwenu,” alisisitiza Lusinde.

Naye Waitara alisema; “nimegombana na Mbowe kwa sababu ya kuzuia mambo ya wananchi yasiende Serikalini. Ili ulete maendeleo lazima uwe na uhusiano na serikali, yeye hilo hataki,” alisema.

Aliongeza kuwa amehamia CCM ili awe karibu na Serikali, jambo litakalosukuma maendeleo ya jimbo lake. Amesema ajenda ya maendeleo sasa sio yake pekee bali ya wabunge wote wa CCM.