http://www.swahilihub.com/image/view/-/4759142/medRes/2109554/-/j7jgfy/-/lihindi.jpg

 

Wagombea ACT wasafiri kilometa 129 kufuata huduma za kimahakama

Mgombea ubunge katika Jimbo la Liwale kupitia ACT- Wazalendo, Mohamed Lihindi  

Na Mwanaja Ibadi

Imepakiwa - Friday, September 14  2018 at  12:38

Kwa Muhtasari

Lengo likiwa kukamilisha taratibu mbalimbali za uchaguzi ili kupata sifa za kugombea

 

Liwale. Mgombea ubunge katika Jimbo la Liwale kupitia ACT- Wazalendo, Mohamed Lihindi amewaomba wananchi wa jimbo hilo kuwa watulivu wakati wagombea wao wakiendelea kukamilisha taratibu mbalimbali za uchaguzi ili kupata sifa za kugombea.

Lihindi alisema hayo jana baada ya kufuata huduma za kimahakama za kusaini kiapo cha mgombea wilaya jirani ya Nachingwea.

Lihindi alisema wamesafiri kilometa 129 kutoka wilaya ya Liwale hadi Nachingwea kufuata huduma za kimahakama baada ya mahakimu wilayani humo kuwa na safari za kikazi nje ya wilaya.

Aliwaomba wananchi kuwa wapole kwani hizo ni changamoto ndogondogo kwenye uchaguzi.

Akizungumzia uchaguzi huo, katibu mwenezi wa chama hicho mkoa, Issa Mbokora alisema chama kimejipanga vizuri kwenye na kinamategemeo makubwa ya kushinda baada ya kumsimamisha mgombea anayekubalika na wananchi. “Sisi hatuingii kwenye uchaguzi kwa lengo la kushiriki tu, lengo letu ni kushinda kwa kishindo,” alisisitiza Nnokota. Wagombea wanne wamepitishwa kuwania jimbo hilo kutoka CCM, Chadema, CUF na ACT.