http://www.swahilihub.com/image/view/-/4706444/medRes/2074973/-/tjct80/-/esta.jpg

 

Waliokamatwa mkutano wa Chadema waachiwa kwa sharti moja

Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko  

Na DINNA MANINGO

Imepakiwa - Friday, August 10  2018 at  11:32

Kwa Muhtasari

Kampeni za Chadema imedaiwa zilikuwa na utata.

 

TARIME, Tanzania

MBUNGE wa Tarime Mjini, Ester Matiko, watu wengine 15 akiwamo mwandishi wa Tanzania Daima, Sitta Tuma waliokuwa wanashikiliwa na polisi wameachiwa kwa sharti la kuripoti leo kituoni.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Polisi Tarime / Rorya, Hennry Mwaibambe alisema watu hao walikamatwa tangu juzi kwa tuhuma za kufanya mkutano usio halali.

Alisema wakiwa kwenye mkusanyiko katika eneo la ofisi ya Chadema wilayani Tarime, Polisi walifika na kuwaomba watawanyike kwa kuwa mkusanyiko huo haukuwa halali lakini walikaidi.

Mwaibambe alisema baada ya kukaidi polisi waliamua kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na bado watuhumiwa hao waliendelea kukakaidi na polisi wakawakamata.

Akizungumzia kisa cha kuzuia kufanya mkutano, Mwaibambe alisema Agosti 8, 2018 alipokea barua kutoka kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi katika Kata ya Turwa kusitisha Kampeni za Chadema kwa kukiuka maadili ya uchaguzi, lakini chama hicho kilikaidi licha ya kupewa barua ya kukitaka kusitisha.

“Sisi tulipewa barua ya zuio la mkutano ikionyesha kuwa Chadema wamekiuka kifungu cha 124 A cha Sheria ya Taifa ya uchaguzi, kwamba wasitishe kampeni hadi Agosti 11 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kampeni.