http://www.swahilihub.com/image/view/-/5118032/medRes/2345510/-/24yvdwz/-/hhyat+pic.jpg

 

Hyatt yafuturisha wanahabari

Na Mwandishi wetu

Imepakiwa - Thursday, May 16  2019 at  13:17

 

Dar es Salaam. Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, imewafuturisha waandishi wa vyombo vya habari mbalimbali ikiwa ni sehemu ya upendo na shukrani kwa tasnia ya habari.

Hafla hiyo iliyofanyika juzi hotelini hapo, pia ilikuwa na lengo la kudumisha uhusiano uliopo.

Akizungumza kwenye futari hiyo, meneja masoko na uhusiano wa hoteli hiyo, Lilian Kisasa alisema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakifanyakazi kwa karibu na tasnia ya habari, hivyo wameona ni vyema mwezi huu wa Ramadhan wajumuike pamoja.

(Bakari Kiango) wanahabari peke yake tulianza kukutana na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na watu wengine wa kada tofauti,” alisema Kisasa.

Kisasa alisema wamekuwa wakifanya hivyo mara kwa mara ikiwa ni sehemu ya kukutana wanatasnia hiyo na kubadilishana mawazo kutokana kazi na mchango mkubwa wanaoufanya kazi jamii.

Meneja Uendeshaji wa hoteli hiyo, Timoth Mlay alisema katika mwezi huu pia, wameandaa futari maalumu kwa ajili ya kufuturisha watu kuanzia saa 12:30 hadi saa 4 usiku ili kuwaleta Watanzania pamoja.

“Nia yetu si kufanya biashara kwanza, bali ni kuwakutanisha pamoja na ndugu zetu walioko kwenye mfungo.Kwa kutambua umuhimu wa mwezi huu menejimenti ilikaa pamoja na kuja mpango wa kuandaa futari maalumu inayopatikana kwa bei rahisi.

Alisema futari hiyo imezingatia vyakula halisi vya Kitanzania ikiwa juhudi za kuunga mkono sera ya utalii ya Tanzania na kwamba bidhaa zinazotengeza vyakula hivyo zinanunuliwa moja kwa moja kutoka kwa wakulima ili kuwajengea uwezo.