Ya Arusha United ni alama tosha ya Changamoto za Ligi Daraja la Kwanza

Imepakiwa - Monday, March 25  2019 at  14:34

 

UCHAMBUZILigi ya Daraja la kwanza ni moja ya ligi ngumu na naamini kwamba inaizidi Ligi Kuu. Katika miaka mingi ambayo mwe-nyewe nilishiriki katika ligi hiyo kama kocha, niliona kwamba ligi hiyo ndiko ambako mpira wa ukweli unapigwa.

Hii inatokana na ukweli kwamba ligi hiyo inajumuisha wachezaji wengi ambao wanainukia na hivyo kuwa bado na nguvu za kutosha kupambana. Aidha, ligi hii ugumu unazidi kwa sababu wachezaji wanapenda kufan-ya vizuri ili wao wenyewe na klabu zao kushiriki Ligi Kuu ya Tanzania, ligi ambayo ndiyo ligi kilele katika nchi yetu. Kutokana na ukweli huo, kumekuwa na jitihada nyingi kwa viongozi wa kla-bu kuhakikisha kwamba timu zao zina-fanikiwa kucheza Ligi Kuu.

Pamoja na ukweli wa umuhimu wa ligi hiyo, michezo ya Ligi Daraja la Kwanza imekuwa na inaendelea kukabiliwa na changamoto nyingi na malalamiko yamekuwa kama vile ni ajenda ya kudu-mu kwani changamoto hizo zimekuwa ni za kila mwaka. Tukio la hivi karibuni la moja ya timu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, Arusha United kutangaza kujiondoa kwenye ligi hiyo kutokana na changa-moto nyingi ambazo wanadai wame-kuwa wakifanyiwa na hatua zozote kutochukuliwa na wahusika..

Uamuzi huo ulimshitua kila mdau wa michezo lakini pamoja na maoni kutofautiana juu ya kuunga au kuup-inga uamuzi huo wa uongozi wa Aru-sha United, ni dhahiri kwamba umetoa ujumbe mahsusi kwa wenye dhamana ya kuuongoza mchezo wa mpira wa miguu.

Kila mmoja wetu anafahamu ni kosa kujiondoa kwenye ligi baada ya kuwa umeianza na adhabu zake ninaamini zinafahamika na viongozi wa Arusha United, lakini pamoja na ukweli huo, bado viongozi wake wameamua kuitoa timu kwenye ligi.

Binafsi ninayaona yafuatayo yame-achwa yaendelee kwa muda mrefu bila hatua za haraka kuchukuliwa.Sheria zinazotawala mchezo hazi-fuatwi kwa makusudiWadau wote ambao huwa wanaan-galia mechi za ligi hii, ni mashahidi kwamba ni kama ligi ambayo haina msi-mamizi.

Taratibu nyingi za sheria zinazou-ongoza mchezo wa miguu hazifuatwi na hivyo haki kutotendeka. Jambo la kujiuliza hapa ni je waamuzi wanakuja na matokeo uwanjani kwa utashi wao au kwa maelekezo. Aidha waamuzi hawa hufanya hivyo kwa sababu wanajua hawatachukuliwa hatua na yeyote.

Viongozi wa timu za daraja la kwanza watakaopata nafasi ya kuisoma makala hii ni dhahiri kwamba watakubaliana na mimi kwamba waamuzi wanapokuja na matokeo mfukoni, huumizwa kwa saba-bu maandalizi na hatimaye ushiriki wa timu kwenye ligi hii yana gharama kub-wa sana hivyo waamuzi wanapofanya dhuluma kwa baadhi ya timu, ghadhabu ya viongozi inaweza kuwa kama hii ya viongozi wa Arusha United.

Ninaamini timu nyingi zinadhulumi-wa na waamuzi na madhara ya jambo hilo ni kuwakatisha tamaa baadhi ya wadau ambao wanapenda kuwa na timu za mpira, hivyo vijana ambao wangenu-faika na juhudi za wadau hao, huikosa huduma hiyo.Baadhi ya wasimamizi wa vituo na makamisaa wanahusika kuiharibu ligiNinaamini kwamba kila kanda ina wasimamizi wa vituo katika maeneo yao kwa niaba ya TFF na Bodi ya Ligi.

Hawa wana dhamana kubwa kuhakiki-sha haki inatendeka. Pamoja na ukweli huo, baadhi ya kanda zimekuwa sugu kwa dhuluma ya timu kutoka kanda nyingine zinapok-wenda kucheza kwao. Mambo haya yamekuwa yakiendelea kwa kipindi kirefu kwenye baadhi ya kanda kwa sababu wanaosimamia kan-da hizo ndiko ambako wapiga kura wao wapo hivyo hufanya kila hila ili timu zao zishinde kama mtaji wa kupata kura uchaguzi unaofuata.

Kutokana na hali hiyo, ushauri wangu kwa TFF ni kwamba viongozi wanaoto-ka kwenye kanda wasisimamie vituo vyao kwa sababu kwa kufanya hivyo, haya yanayoendelea hayatakwisha.

TFF itafute namna nyingine bora ya usimamizi. Aidha, baadhi ya makamisaa wamei-fanya kazi hiyo ni ya kujipatia kipato zaidi ya kile wanachopata na wao pia husababisha haki kutotendeka.

Ushauri wangu kwa makamisaa ambao matukio mengi yametokea kwe-nye mechi walizosimamia na taarifa hazikuonyesha hivyo, waondolewe kwa manufaa ya mpira.

Hatuwezi kuendelea kulea uozo, matukio yanafanyika lakini hayamo kwenye ripoti za waamuzi.Ya Arusha United ni alama tosha ya Changamoto za Ligi Daraja la KwanzaPamoja