http://www.swahilihub.com/image/view/-/1416578/medRes/365378/-/y7thhkz/-/sato53.jpg

 

AUNTIE POLLY: Je, ni sawa kulala ukiwa umevalia sidiria?

Wachumba

Wanandoa wakifurahi pamoja wakiwa kitandani. Picha/MAKTABA 

Na PAULINE ONGAJI

Imepakiwa - Wednesday, December 6  2017 at  15:41

Kwa Muhtasari

Je, ni sawa kulala ukiwa umevalia sidiria? Jackline, 18, Nairobi

 

Ushauri

Bila shaka umeskia fununu mbaya na nzuri kuhusu athari za kulala na sidiria, lakini ukweli ni kuwa hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha tetesi hizi.

Kulingana na wataalam hakuna ubaya wa kulala ukiwa umevalia sidiria hasa ikiwa haikunyimi starehe. Kuna baadhi ya madaktari wanaoshauri kulala na mavazi haya ikiwa unakumbwa na maumivu katika sehemu hii.

Kulala na sidiria kamwe hakuchangamshi matiti yako wala kuyalegeza, na kamwe hakuwezi sababisha kansa wala kufanya yasikue. Baadhi ya wanawake huvalia sidiria wakilala kwani wanahisi starehe wakifanya hivyo.

Kila wakati hata hivyo unapaswa kuchagua sidiria inayokusitiri vyema na isiyokukaba.

Mpenzi wangu tayari ashashiriki ngono na watu kadha kwani amenizidi umri. Kwa sasa anataka tuchukue hiyo hatua ya kushiriki mahaba lakini nina hofu kwani sijui iwapo ameambukizwa maradhi ya zinaa, na pia sitaki kushika mimba. Nitajuaje iwapo ameambukizwa maradhi ya zinaa bila kumuuliza?
Stella, 21, Nairobi

Ushauri

Uko sawa kufikiria kuhusu uwezekano huu. Hakuna jinsi ya kumwangaalia mtu na kujua iwapo anaugua maradhi ya zinaa.

Wakati mwingine hata watu wanaougua maradhi ya zinaa hawafahamu kuwa wao ni wagonjwa. Kushiriki mahaba ni hatua kubwa maishani kwani kuna hatari ya kuambukizwa maradhi ya zinaa, kushika mimba, au vyote viwili, suala ambalo bila shaka lina uwezo wa kubadilisha maisha yako.

Kondomu ndio njia bora ya kuzuia mimba na maradhi ya zinaa na hivyo ikiwa unahisi kana kwamba uko tayari kuchukua hatua hii hakikisha kuwa unatumia vyema kinga kila mara. Lakini unapaswa kujua kuwa kondomu haikuhakikishii usalama kabisa, na ndio sababu lazima umhusishe mwenzio kwa kuzungumza naye kabla ya kushiriki ngono.

Ikiwa mwenzako amekueleza ukweli kuhusu mahusiano yake ya awali, hiyo ni ishara kwamba atakuwa muwazi ukimzungumzia kuhusu hatari zinazotokana na kushiriki ngono. Unaweza anza kwa kumuuliza iwapo amewahi pimwa kubaini ikiwa ana maradhi yoyote ya zinaa.

Ni kawiada kukumbwaa na hofu hasa ikiwa unazungumzia suala hili kwa mara ya kwanza, lakini ikiwa anakupenda na anakujali hatakumbwa na tatizo lolote ukizugumza naye kuhusiana na suala hili.

Ikiwa umewahi shiriki ngono awali, wewe na mwezio mwaweza andamana kwenye kituo cha kiafya na kupimwa pamoja. Mkiwa hapo uliza kuhusu mbinu za upangaji uzazi kwani kuna uwezekano wa kushika mimba hata ukitumia kinga hasa ikiwa hamtumii jinsi inavyofaa.