http://www.swahilihub.com/image/view/-/4927408/medRes/2219317/-/sj1ojo/-/Mandojo.jpg

 

Baada ya kuvunjiwa nyumba, Mandojo aamua kujenga ghorofa

Mandojo 

Na Nasra Abdallah

Imepakiwa - Wednesday, January 9  2019 at  12:04

Kwa Muhtasari

Wakati mwingine unapitia matatizo ili uweze kujiongeza zaidi

 

 

Msanii wa Bongo Fleva, Mandojo aliyewahi kutamba na kundi la Daz Nundaz amesema hasira za kubomolewa nyumba yake ameamua ajenge ghorofa kwenye kiwanja alichohalalishiwa na Serikali.

Mandojo alibomolewa nyumba iliyokuwa maeneo ya Mbweni mwaka jana baada ya kudaiwa kujenga kwenye eneo lenye mmiliki mwenye hati halali.

Mgogoro huo uliingiliwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni kipindi hicho, Ali Hapi kwa kumtafutia eneo jingine alilomilikishwa kihalali.

“Nimetoka kule stoo nilikokuwa naishi sasa nimepanga nyumba, wakati mwingine unapitia matatizo ili uweze kujiongeza zaidi, kwa lililonitokea siwezi kijilaumu zaidi naona limenipa hamasa ya kutafuta zaidi,” alisema Mandojo ambaye aliwahi kutamba na wimbo wa Dingi akiwa na mwenzake Domokaya.