http://www.swahilihub.com/image/view/-/4756260/medRes/2107702/-/12na6no/-/ua.jpg

 

Macha: Baadhi ya madereva hutenga bajeti kwa ajili ya kulipa faini barabarani

Ajali ya gari 

Na Shija Felician

Imepakiwa - Wednesday, September 12  2018 at  16:28

Kwa Muhtasari

Askari wa usalama barabarani watakiwa kuwakamata madereva wanaovunja sheria kwa kuwa wengi huzivunja kwa makusudi

 

 

Kahama. Idadi ya ajali za barabarani zitokanazo na watu kugongwa na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda au kugongana wenyewe, zimepungua mjini hapa mkoani Shinyanga kutoka zaidi ya 20 kwa wiki hadi nne.

Hayo yalielezwa juzi na mkuu wa usalama barabarani kutoka Polisi Kahama, Joseph Mgeri wakati akitoa elimu kwa walemavu wasiosikia kutoka Chama cha Viziwi Tanzania (Chavita).

Alisema hivi sasa ajali zinatokea nne kwa wiki tofauti na mwaka jana ambako zilikuwa zikitokea kati ya 20 na 30.

Naye mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha aliwataka askari wa usalama barabarani kuacha mzaha wakati wa kukamata madereva wanaovunja sheria kwa kuwa wengi huzivunja kwa makusudi.

Macha alisema kuna madereva wanapoandaa safari hutenga bajeti kwa ajili ya kulipa faini.