Bangi na Sanaa

Na Idd Ninga wa Tengeru

Imepakiwa - Wednesday, March 27  2019 at  10:31

 

Wajisifu wakivuta, bangi yawasisimua,

Mwisho siku kujutia, vichwa ikiwasumbua,

Washindwa kufurukuta, wengine kujinunia,

  Bangi na sanaa noma, kama mkijivutia.

Bangi balaa kuvuta, sifa inaharibia,

Inabomoa ukuta, mandadi wa sanaa,

Ipo siku ni kujuta, na polisi kuingia,

  Bangi na sanaa noma, kama mkijivutia.

Utaona sitasita,kichwani ikikolea,

Hauwezi kufurukuta, hakika nakuambia,

Mgambo wa kutafuta, virungu waje kutia,

  Bangi na sanaa noma, kama mkijivutia.

Kidogo unapovutadamu unaishtua,

Na mishipa iso sita, kichwani moshi ingia,

Ukijua umepata, kumbe imekupatia,

  Bangi na sanaa noma, kama  mkijivutia.

Maji kioo wajita,  kumbwa watuharibia,

Naona wakunja ndita, punde ninamalizia,

Kama uliwahi vuta, najua utachukia,

  Bangi na sanaa noma kama mkijivutia.

Mwisho