http://www.swahilihub.com/image/view/-/4396356/medRes/1941003/-/13fe3y6/-/pierce.jpg

 

Barbara Pierce Bush kiafya abaki tu kumuachia Mungu

Barbara Bush

Picha ya maktaba ya Julai 15, 2013, ya aliyekuwa Mama wa Taifa nchini Marekani Bi Barbara Bush katika hafla jijini Washington, DC. Picha/MAKTABA 

Na MWANGI MUIRURI na MASHIRIKA

Imepakiwa - Monday, April 16  2018 at  18:01

Kwa Muhtasari

Barbara Pierce Bush hatasaka matibabu tena bali atangoja hatima ya Mungu atakavyoamua.

 

BAADA ya kuugua kwa muda mrefu na akawa anakesha katika hospitali kadhaa nchini Marekani, familia ya aliyekuwa Rais, George Bush, sasa imetoa taarifa ikisema kuwa mamake, Barbara Pierce Bush hatasaka matibabu tena bali atangoja hatima ya Mungu atakavyoamua.

Barbara Bush pia alikuwa mama wa taifa la Marekani baada ya kuwa mkewe rais na kisha akamzaa mwana aliyeishia kuwa rais.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari,familia hiyo imesema kuwa mama huyo ambaye amekuwa akiugua maradhi kadhaa hatari kwa maisha ya binadamu na kwa sasa ako na uzee wa miaka 92 amesalimu amri ya maisha.

Msemaji wa familia hiyo, Jim McGrath katika taarifa ya Jumapili amesema kuwa kwa sasa familia ya Barbara Bush inashukuru Mungu kwa kuwapa maisha na mama huyo na kwa sasa itazingatia kumfariji katika kitanda chake cha kuugua na kumwonyesha mapenzi ya kuwa wa familia moja nao.

Magonjwa ambayo amekuwa akitibiwa yanajumuisha thyroid, ugonjwa wa moyo na pia vidonda vya tumbo.

“Barbara Bush kwa wengi amekuwa ngome ya kuwa ngangari katika hali yake ya kiafya na badala ya kuihurumia, amekuwa akihurumia wengine walio katika changamoto za kimaisha,” taarifa hiyo yasema.

Anasema kuwa kwa sasa mama huyo amezingirwa na familia yake pana na ambayo kwa maombi wako pamoja na pia katika kumdhihirishia kuwa hayuko peke yake akiiendelea kutegemea imani yake thabiti kwa Mungu.

Imesema kuwa Barbara Bush kwa sasa hataenda hospitalini tena na atakuwa kitandani katika chumba chake ndani ya Mji wa Houston.

 Barbara Bush ni wa pili kuwa mama wa taifa na kisha kuwa mama kwa rais wa taifa katika taifa hilo, kando na Abigail Adams ambaye alikuwa mkewe rais John Adams aliyekuwa rais wa pili wa Marekani na kisha akawa mama kwa rais wa sita wa taifa hilo, John Quincy Adams.

Hapa Kenya, Mama Margaret Kenyatta naye ana usawa huo wa kihistoria ambapo alikuwa mke wa rais wa kwanza, Jomo Kenyatta na kisha kwa sasa ni mama kwa rais wa nne, Uhuru Kenyatta.

Barabra aliolewa na George H.W. Bush januari 6, 1945 na wakajaliwa watoto sita na hadi sasa, ndio wanashikilia rekodi ya kuishi pamoja katika ndoa kati ya marais wote wa Marekani.

Miaka minane baada ya kutoka Ikulu ya Marekani baada ya awamu yao uongozini kutamatika, walirejea tenka kushuhudia mtoto wao, George W Bush akilishwa kiapo cha kuwa rais wa Marekani katika ikulu iyo hiyo akiwa Rais wa 43.

Mama Barabara Bush anafahamika vyema na nembo yake ya nywele nyeupe kichwani na mkufu wake wa thamani shingoni.

Nywele hiyo ilianza kuota mvi miaka ya 1950 na ashawahi kupoteza mtoto wake kwa ugonjwa wa Leukemia - Pauline Bush aliyeaga akiwa na miaka mitatu Oktoba 1953.

Maadili

Alikataa katakata kupaka nywele yake rangi ili ibakie kuwa ya kawaida ya Uzungu akisema kuwa hakuwa vyema kwa maadili na akaamua kubakia na taswira ya “nyanya wa kila mtu.”

Bwanake ambaye alikuwa rais wa 41 wa Marekani kati ya 1989 na 1993 pia ako katika hatari ya kiafya ambapo hutumia kijigari cha kusukumwa kutembea na kwa sasa ako na miaka 93.

Mama Bush alizaliwa 1925 katika jimbo la Rye, New York na akasomea katika Milton Public School huko Rye kuanzia 1931 hadi 1937 na kisha Rye Country Day School hadi 1940 na hatimaye Ashley Hall High School.

Babake mzazi alikuwa mchapishaji wa majarida ya McCall's na Redbook na aliolewa katika kanisa la Kipresibeteria la Rye akiwa na miaka 19.

 Ameandika vitabu kama "C. Fred's Story" na "Millie's Book," vikiwa ni kumbukumbu zake na majibwa yake.

 Akon a wakfu wa Bush ambao huzingatia sana elimu kwa wanyonge wa ulimwengu na ambao unakadiriwa kuwa tayari umetumia bajeti ya dola 40 milioni kufadhili miradi  1,500 ya kielimu.