http://www.swahilihub.com/image/view/-/4912912/medRes/2209688/-/o3efjw/-/bianga.jpg

 

Bianga: Anapania kumpiku mwigizaji Ini Edo wa Nigeria

Veronica Nyangai Muliro

Mwigizaji Veronica Nyangai Muliro maarufu Bianga. Picha/JOHN KIMWERE  

Na JOHN KIMWERE

Imepakiwa - Friday, December 28  2018 at  14:14

Kwa Muhtasari

Veronica Nyangai Muliro maarufu Bianga analenga kuigiza katika muvi ya uhalifu iitwayo 'The Private' chini ya Onfon Media Productions produsa akiwa Peterson Kariuki.

 

NDIYO ameanza kupiga ngoma anakolenga kukwea milima na mabonde kusudi kutinga levo ya kimataifa katika tasnia ya filamu na muvi.

Huyu sio mwingine bali ni Veronica Nyangai Muliro; mwigizaji anayekuja na pia mshauri wa masuala ya hoteli. 

Veronica, 28, anayejulikana kama Bianga na wafuasi wake amehitimu kwa shahada ya digrii kuhusu masuala ya hoteli.

''Ninaamini nitafaulu kupiga hatua katika uigizaji kufikia sasa hamna filamu niliyoshiriki na kuonyeshwa kwenye televisheni,'' anasema Bianga na kuongeza kwamba ndiyo safari inaanza. Kwenye masuala ya ushauri anafanya kazi na hoteli tofauti ikiwamo: Anasema kati ya projekti zake, mapema mwaka 2019 atashiriki muvi ya uhalifu iitwayo 'The Private' chini ya Onfon Media Productions produsa akiwa Peterson Kariuki.

''Nitashiriki nafasi ya 'Bosi' ikiwa ni mwanya niliyoupata baada ya kuonekana kwenye muvi ya 'Married in Kenya' iliyofanyiwa kazi na Connie Kabarry Production,'' alisema na kuongeza kwamba ana imani nafasi ya ubosi itamsaidia kutambulika na wengi.

Kwenye muvi ya 'Married in Kenya' alishirikiana na mastaa watajika wa Kinigeria akiwamo Emeka Ike na Paul Sambo kati ya wengineo.

Anasema anatosha mboga katika uigizaji ingawa mwaka 2014 alijipata akiyeyusha imani katika ulingo huo. Kupitia bradi hiyo wameingia dili na wasanii tofauti wa Nollywood ambapo mwaka 2019 watasafiri nchini Nigeria kupokea mafunzo ya uigizaji kisha kushiriki muvi kadhaa. 

''Tunahitaji kupenya na kufanya kazi kwa kushirikiana na wenzetu katika mataifa tofauti kama Tanzania, Uganda na Nigeria ili kupaisha tasnia ya filamu na muvi hapa Kenya. Bila shaka kwa ushirikiano huo tufajifunza mengi kuhusu sanaa ya uigizaji.''

Ingawa ndiyo ametinga mwaka mmoja tangu aanze kujituma katika burudani ya filamu analenga kumpiku staa Iniekim Edo maarufu Ini Edo wa muvi za  Kinaijeria (Nollywood) pia Priyanka Chopra Jonas wa Uigereza.

Chipukizi huyu hupagawishwa na muvi kama 'Code of Silence' na White Witch' zake Ino Edos huku kwa Priyanka Chopra Jonas akipenda kutazama 'Quantico,' na 'Krrish' kati ya zinginezo.

Moyo wa kusaidia

Anasema miaka ijayo analenga kuanzisha wakfu wa masuala ya hoteli, wakfu wa masuala ya kijamii pia wakfu wa uigizaji ili kusaidia watu tofauti.

Alidokeza kwamba sekta ya uigizaji hapa Kenya inapiga hatua kinyume na ilivyokuwa miaka ya awali.

Anazitaka serikali za Kaunti bila kuweka katika kaburi la sahau serikali ya kitaifa kuwazia sanaa ya uigizaji.

Hata hivyo binti huyu siyo mchoyo wa mawaida. Anawahimiza wenzie kamwe watokubali kuangushwa na wenzao pia marafiki zao bali wajiaminie kwa chochote wanachoshughulikia. Pia wajiheshimu na kuonyesha nidhamu nzuri nyakati zote bila kuweka sahau kumwomba Mungu.