http://www.swahilihub.com/image/view/-/4928714/medRes/2220037/-/k63um0/-/satta.jpg

 

Boateng yamkuta ya Byrant kwa Melissa

Prince Kevin Boateng akiwa na mke wake, Melissa Satta 

Na Thomas Matiko

Imepakiwa - Thursday, January 10  2019 at  09:58

Kwa Muhtasari

Ndoa yake Satta na Boateng kwa sasa ipo juu ya mawe

 

MKE wake kiungo mshambuliaji wa Sassaulo, Prince Kevin Boateng, Melissa Satta ndiye aliyekuwa chanzo cha kutaka kuvunjika kwa ndoa ya mchezaji kikapu maarufu duniani, Kobe Byrant.

Taarifa hizi zimefichuka baada ya kuripotiwa ndoa yake Satta na Boateng kwa sasa ipo juu ya mawe huku kukiwa na hofu kuwa wanandoa hawa watakuwa wakichepukiana.

Hali hiyo imezua kumbukumbu za mwaka 2011 na nusura aivunje ndoa ya Kobe, baada ya kunaswa na kamera akiingia kwenye hoteli ambayo staa huyo wa kikapu alikuwepo.

Tetesi zilidai wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimya kimya. Kipindi hicho Melissa alipata umaarufu kutokana na skendo yake ya kumchepukia mpenzi wake wa zamani Christian Vieri. Hivyo, ikawa rahisi kwa mke wake Kobe, Vanessa kusadiki ripoti hizo na kuomba talaka fasta tu.

Hata hivyo, baaada ya wiki chache za mazungumzo, Kobe alibadili mawazo Vanessa na kuendelea kuwa pamoja.

Lakini kwa sasa zimeibuka taarifa huenda kule Milan anakoishi akawa anamchepukia Boateng na mmoja wa watu mashuhuri, japo haijathibitishwa.

Boateng na Melisa waliooana 2016, lakini hawaishi pamoja wakitengeneshwa na kilomita kadhaa. Boateng yupo mjini Sassaulo iliko klabu anayoichezea huku mke wake pamoja na mwanaye wa kiume waliyejaliwa kumpata mwaka 2014, wakiendelea na maisha kwenye jiji la maraha la Milan.