http://www.swahilihub.com/image/view/-/2798426/medRes/981701/-/635xgtz/-/DNCSNGILU3003A.jpg

 

Charity Kaluki Ngilu: Alipata umaarufu mkubwa wakati akiitwa 'Mama Rainbow'

Charity Ngilu

Bi Charity Ngilu akihutubia wanahabari awali. Picha/SALATON NJAU 

Na MWANGI MUIRURI

Imepakiwa - Wednesday, February 14  2018 at  06:59

Kwa Muhtasari

Charity Kaluki Ngilu akiwa mwanasiasa mwenye tajriba hapa nchini Kenya kwa sasa ni gavana wa Kitui.

 

CHARITY Kaluki Ngilu akiwa mwanasiasa mwenye tajriba hapa nchini Kenya kwa sasa ni gavana wa Kitui.

Ni mwanasiasa ambaye mkondo wake wa kisiasa umejaa mawimbi makali ya kumwangazia kama sio tu mwanasiasa wa kawaida, bali pia ambaye aliye na uwezo wa kujiingiza kwa lindi moja baada ya lingine na abakie amesimama wima kisiasa.

Mzawa wa Kaunti hiyo ya Kitui miaka 66 iliyopita, anatazamiwa kutimiza umri wa miaka 70 akimaliza awamu yake ya kwanza ya ugavana na iwapo atawania kwa awamu ya pili na ya mwisho kwa mujibu wa katiba, atimizie miaka 76 afisini.

Kwa sasa, yuko katika hatari ya kufunguliwa masjhtaka kwa madai kuwa hivi majuzi alichochea wafuasi wake kuchoma gari la mfanyabiashara wa Kaunti ya Kiambu kwa ‘makosa’ ya kushiriki biashara ya makaa katika eneo hilo la Kitui.

Inadaiwa kuwa alitoa matamshi ambayo hayana msingi wa nidhamu ya utaifa ambapo anasemwa alisema wafanyabiashara hao wakionekana katika Kaunti hiyo ya Kitui, washambuliwe.

Ngilu sio mara yake ya kwanza anajipata katika utata wa kisiasa kwa kuwa mwaka wa 2007 alitoweka na chama cha Narc ambacho Rais wakati huo akiwa Mwai Kibaki alikuwa awanie nacho awamu ya pili afisini.

Ilibidi wandani wa Mzee Kibaki waunde chama cha Narc Kenya haraka haraka ili kunusuru jahazi lake la ugombezi, ingawa kuwa hata hicho chama kililemewa kujipa sura ya kitaifa na ndipo akawania kwa chama kipya cha Party of National Unity (PNU.)

Ni uyu huyu Ngilu ambaye mwaka wa 2006 alimfanya aliyekuwa waziri wa usalama wa Ndani, John Michuki atorokee usalama wake kutokla mlango wa nyuma wa afisi yake i0liyokuwa katika jumba la Harambee, Jijini Nairobi.

Michuki alikuwa amemsuta Bi Ngilu kama mwanamke asiye na msimamo wa kufuatwa na aliyekuwa akiyumbayumba kimaamuzi kama mcheza densi mtindo wa 'Wathi wa Mukamba'.

Ngilu alikusanya wanawake wafuasi wake kuvamia jumba hilo la Harambee kusaka Michuki amuambie pole kwa kumwangazia kwa msingi huo na ndipo Michuki alitoweka.

Ngilu alizaliwa kiatika familia kubwa ya watoto 13 na ambapo alikuwa wa tisa katika familia ya mchungaji .

Ngilu akaolewa kwa Michael Mwendwa katika miaka ya 1980 lakini akaaga dunia mwaka wa 2006 akiwa baba wa watoto watatu.

Taaluma yake ni karani ambapo alihudumu katika majukumu ya taaluma hiyo kwa benki kuu (CBK).

Anasemwa kuwa mwekezaji shupavu ambapo ako na biashara kadhaa ambazo utajiri waike unaangaziwa kuzidi 3 bilioni.

Mwaniaji urais wa kike

Alikuwa mwaniaji wa urais wa kwanza mwanamke katika historia ya taifa hili ambapo mwaka wa 1997 alishindwa pamoja na wote ndani ya upinzani na aliyekuwa rais Daniel arap Moi.

Alijiunga na siasa kama mbunge wa Kitui ya Kati mwaka wa 1992 alipochaguliwa.

Alihudumu kama waziri katika serikali ya Mweai Kibaki ambapo aliwajibishwa majukumu ya wizara wa Afya na pia maji kabla ya kunaswa na mtego wa ufisadi na katika harakati hizo za kujitakasa, akang’oka serikalini.

Alijiunga tena na siasa za ubunge na akafanikiwa kutwaa uwaziri katika seriikali ya UhuRuto olakini mwaka wa 2015 akang’olewa tena kwa madai ya ufisadi.

Ndipo akawania ugavana na akautwaa hivyo basi kuingia katika historia nyingine ya kuwa miongoni mwa magavana watatu wanawake wa kwanza katika historia ya Kenya kuchaguliwa.

Akifahamika kama Mama Rainbow au Masaa, hivi ndivyo Ngilu anarejelewa na wachanganuzi: “Mara kwa mara amekuwa akizua utata wa kisiasa kwa msingi wa mashindano lakini kwa hili la uchochezi amejiangazia kwa sura tofauti sana na ya kushtua.”

Hayo ni maneno yake Profesa Ngugi Njoroge, mchanganuzi wa siasa za Mlima Kenya katika taswira ya kitaifa.