Dawa za asili hutibu vidonda vya tumbo

Na  Mwandishi wetu

Imepakiwa - Friday, April 5  2019 at  10:12

 

Watu wengi hawajui kuwa vidonda vya tumbo husababishwa na mienendo mibaya ya maisha yetu na mfumo wa chakula cha kila siku.

Dawa kama Omeprazole, Tagament, Cimetidine na zingine nyingi za hospitali huwa zinapunguza maumivu tu kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Dawa hizi hupunguza asidi (tindikali) ambayo huharibu kuta za mfuko wa chakula.

Zinazuia asidi bila kushugulika na chanzo cha kuongezeka kwa hiyo tindikali.

Hivyo bila kuondoa chanzo kinachosababisha kuongezeka kwa asidi hiyo, huwezi kupona.

Pengine huamini kuwa vidonda vya tumbo vinaweza kupona vikaisha.

Dawa za vidonda vya tumbo zinatakiwa zitumike pale panapohitajika tu, siyo maisha yako yote.

Kwa kawaida dawa za hospitali mara nyingi huja na maudhi mbalimbali kwani ni dawa ambazo zimetengenezwa kwa kemikali.

Dawa pekee ambazo ni rahisi na za uhakika na hazina madhara ni dawa asili tu.

Changamoto kubwa kwa hapa nchini, huduma hii ya tiba asili haijapata wataalamu wengi waliobobea wa kutoa bidhaa bora na zenye kufanyiwa utafiti wa kutosha na zenye kiwango cha kimataifa.

Tiba ya vidonda vya tumbo

Kuna aina nyingi za dawa za vidonda vya tumbo katika tiba asili tena zenye kusababisha kupona kabisa.

Changanya mdalasini, Khurinjani, Tangawizi, Habasoda na manjano, vyote viwe na ujazo sawa.

Au, chota kijiko kimoja na asali vijiko vitatu kisha weka kwenye glasi ya maziwa au uji na unywe kutwa mara tatu.

Hakikisha hizo dawa unazipata zikiwa mpya.

Epuka dawa zilizo kaa dukani miaka mingi, hazina nguvu.

Vyakula vya kuepuka

Epuka kula vyakula vyenye viungo vingi, kinywaji chenye kafeini, pombe ya aina yoyote, vyakula vya ngano nyeupe kama mikate na vinywaji vya sukari nyingi.

Hii ni kwa sababu ulapo au unywapo sukari nyingi inalisha bakteria wabaya na hatimaye bakteria wazuri wanakufa. Epuka pilipili na vitu vyenye ukali kama ndimu, limao na ukwaji.

Mwandishi wa makala haya ni daktari wa tiba mbadala