http://www.swahilihub.com/image/view/-/4661636/medRes/2043779/-/o0cl4fz/-/diamond.jpg

 

Diamond adaiwa kuiba vipande vya wimbo wake mpya

Diamond Platnumz  

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Friday, July 13  2018 at  16:42

Kwa Muhtasari

Kwa sasa video hiyo inaendelea kukimbiza katika mitandao

 

Dar es Salaam. Wimbo mpya wa Diamond Platnumz unaitwa Baila akimshirikisha mpiga zeze maarufu wa Marekani, Miri Ben Ari umezua gumzo baada ya video yake kufananishwa na wimbo wa Shahrukh Khan katika filamu ya Jab Tak Hai Jaan.

Baada ya Diamond kutambulishwa rasmi wimbo wa Baila, kumekuwa na maoni mbalimbali katika mitandao ya kijamii kwa  mashabiki wakimtuhumu Diamond kuwa katika Video ya wimbo huo ame kopi baadhi vipande kutoka video ya wimbo Shahrukh Khan.

Katika filamu ya Kihindi inayokwenda kwa jinala “Jab Tak Hai Jaan” ambayo iliachiwa mwaka 2012, katika baadhi ya nyimbo katika filamu hiyo kama kawaida ya Wahindi kuna wimbo unaoitwa Saans.

Katika video hiyo, kuna baadhi ya vipande kama mwanzo kabisa ambapo anaonekana Katrina Kaif akiwa anakimbia akikatiza mitaa mbalimbali ya London kama filamu ilivyoelezwa na kwenda kumkumbatia Shah Rukh Khan.

Katika video ya Diamond kama umetazama mwanzoni kabisa imeanza hivyo hivyo pia.

Lakini isitoshe, kuna baadhi ya vipande vingine kama, sehemu ambayo Diamond yupo na mrembo kwenye chumba cha kupigia simu, nayo katika filamu ni hivyo hivyo.

Pia, kuna sehemu katika daraja, nayo pia imeonesha hivyo hivyo na baadhi ya maeneo kadhaa ambapo hakika video ya Diamond inaonesha wazi kuwa imefanyika katika mitaa ya London, Uingereza.

Filamu nayo ilifanyika kwa sehemu kubwa London, Uingereza na mfanano wa maeneo kwa kiasi kikubwa unaashiria kuwa inawezekana kuna kitu kimefanyika.

Meneja wa Diamond, Babu Tale alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo simu yake haipokelewi.

Kwa sasa video hiyo inaendelea kukimbiza katika mtandao wa Youtube, huku ikiwa inashika namba moja katika video zinatafutwa.