Eric Omondi amshukuru Diamond Platnumz

Eric Omondi

Msanii Eric Omondi (mwenye kinasa sauti) atumbuiza jijini Nairobi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mitandao ya Kijamii mnamo Juni 30, 2015. Picha/WYCLIFFE MUIA 

Na THOMAS MATIKO

Imepakiwa - Friday, February 17  2017 at  15:32

Kwa Mukhtasari

Eric Omondi ambaye ndani ya miezi miwili ijayo atakuwa na shoo yake ya televisheni nchini Tanzania, sawa na ile ya mlezi wake Churchill Show, amemshukuru sana staa wa Bongo Flava, Diamond Platnumz kwa kumfungulia milango huko kwao na kumfanya akubalike kinoma.

 

CHALE wa nyumbani Eric Omondi ambaye ndani ya miezi miwili ijayo atakuwa na shoo yake ya televisheni nchini Tanzania, sawa na ile ya mlezi wake Churchill Show, amemshukuru sana staa wa Bongo Flava, Diamond Platnumz kwa kumfungulia milango huko kwao na kumfanya akubalike kinoma.

Siku kadha zilizopita alipofanya mahojiano na kipindi cha The Trend, Erico alifunguka jinsi Diamond alivyomsaidia kupenya kwenye soko la Tanzania na anasema hana shauku na upendo pamoja na sapoti anayoipata kutoka kwa Watanzania.

Mtangazaji Larry Madowo alipomuuliza ni vipi ameweza kuwa maarufu nchini Tanzania alisema, “Aaah! Diamond. Nilikutana na Diamond yapata miaka miwili mitatu iliyopita Mombasa baada ya mimi kufanya remix ya wimbo wake Nasema Nawe na nikauita ‘Nabeba Mawe’ na akapenda. Hivyo nilipokutana naye akaniambia, ‘aisee we nimekutafuta sana bana’ na hapo akanialika kwa shoo moja kubwa kabisa Tanzania ya Zari All White Party aliyonitaka kuwa mfawidhi (MC). Ni shoo iliyofanikiwa kwani nilipokwenda nilijua runinga na redio zote za huko zingelikuwa pale hivyo nikajituma na si ajabu matunda yake ndiyo haya sasa,” akafichua.