http://www.swahilihub.com/image/view/-/4756078/medRes/2107556/-/nm9ubi/-/puliza.jpg

 

Halmashauri yaanza kukabiliana na ugonjwa wa malaria

Mkazi akikabiliana na ugonjwa wa malaria kwa kupulizia viuatilifu katika bwawa  

Na Mahingo Mwemezi

Imepakiwa - Wednesday, September 12  2018 at  14:56

Kwa Muhtasari

Yapulizia viuatilifu katika makazi ya watu na mabwawa

 

 

Kakonko. Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, imeanza kutekeleza mkakati wa kukabiliana na ugonjwa wa malaria kwa kupulizia viuatilifu katika makazi ya watu na mabwawa.

Akizindua zoezi hilo juzi, msimamizi kitengo cha malaria mkoani hapa, Christopher Mshana alisema tafiti zilizofanywa karibuni zinaonyesha mkoa huo unaongoza kwa maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa asilimia 24 zaidi ikiwa ni wilaya ya Kakonko.

Aliongeza kuwa dawa kwa ajili ya kunyunyizia mazalia ya mbu zipo hivyo kinachohitajika ni utekelezaji kuhakikisha wanafikia lengo lililokusudiwa.

Naye mganga mkuu wa wilaya hiyo, Dk Joseph Tutuba aliwasihi watakaopewa kazi ya kunyunyizia viuatilifu hivyo katika makazi ya watu kuhakikisha wanazingatia taratibu zote ili kuepuka mvutano baina yao na wananchi.