http://www.swahilihub.com/image/view/-/4929352/medRes/2220416/-/13ym4hm/-/hapi.jpg

 

Hapi azikalia kooni kampuni kulipa bili

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi 

Na Berdina Majinge, Mwananchi

Imepakiwa - Thursday, January 10  2019 at  15:19

Kwa Muhtasari

Kampuni zinazodaiwa fedha zinatakiwa kulipa haraka iwezekanavyo

 

Bmajinge@Mwananchi.co.tz

Iringa. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote mkoa huo kuziandikia bili kampuni zinazojishughulisha na usimikaji nguzo ili ziweze kulipa mapato kwa mujibu wa sheria.

Alitoa agizo hilo jana katika kikao cha kujadili masuala ya mapato na wakurugenzi, wakuu wa wilaya na watendaji wa mkoa wa Iringa.

“Kampuni zinazodaiwa fedha zinatakiwa kulipa haraka iwezekanavyo bila kigugumizi mara baada ya kupokea bili kutoka kwa wakurugenzi ili fedha hizo zielekezwe kwenye shughuli za maendeleo ya mkoa huo,” alisema.

Alisema mapato yote yatakayokusanywa yaelekezwe kwenye shughuli za maendeleo kama ujenzi wa shule, maji na afya ili wananchi wa mkoa huo wafaidi matunda ya rasilimali walizonazo.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa Iringa wenye uwezo wa kuanzisha viwanda vya kutibu nguzo na kuahidi kuwapigania kupata tenda.