http://www.swahilihub.com/image/view/-/4801102/medRes/2137408/-/5yw2ea/-/makonda.png

 

JKT wayamezea mate makontena ya Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Thursday, October 11  2018 at  11:50

 

Mafinga. Baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutangaza kuanza kufanya utaratibu wa kuyatoa bandarini makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili kuyagawa bure, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limeomba kukumbukwa katika mgao huo.

Septemba 23 Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere alilieleza Mwananchi kuwa makontena hayo yatagawiwa bure.

Ombi la JKT lilitolewa juzi wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa wakati Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi akizindua jengo jipya la utawala la Shule ya Sekondari Kawawa.

Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu alimuomba Dk Mwinyi azungumze na waziri mwenzake mwenye dhamana na makontena hayo ili sekondari hiyo ambayo JKT ni mmiliki wake, isipitwe na mgao huo.

Dk Mwinyi alisema kama samani hizo bado hazijagawiwa wizara yake itakuwa moja ya taasisi zitakazopata mgao huo.