http://www.swahilihub.com/image/view/-/4803436/medRes/2138908/-/122uyey/-/karoti.jpg

 

Jenga tabia ya kula karoti mbichi uone faida zake

Karoti mbichi  

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Friday, October 12  2018 at  17:31

Kwa Muhtasari

Weka nguvu zako katika ulaji wa karoti mbichi

 

Virutubisho vingi tunavipata katika matunda, mboga za majani, samaki, nyama na vyakula vingine vingi huku tukitumia karoti kama kiungo katika mapishi.

Licha ya karoti kuzuia maradhi mbalimbali yanayosababishwa na kasoro ya ugawanyikaji wa seli mwili, bado jamii haijaipa thamani karoti katika ulaji unaofaa, badala yake karoti imeishia kuwa kama kiungo katika vyakula mbalimbali kwa baadhi ya familia. Achana na habari za kuitumia karoti kama kiungo katika upishi wako, bali weka nguvu zako katika ulaji wa karoti mbichi kwa sababu njia nzuri ya kupata virutubisho kwenye karoti ni kula mbichi na sio iliyoiva.

Wataalamu wa masuala ya lishe wanabainisha kuwa karoti iliyopikwa hupoteza virutubisho vyake na kwamba ikitunzwa katika hali ya chini ya kiwango cha joto, karoti inazuia thamani ya virutubisho yake kwa muda wa miezi mitano hadi sita. Moja ya faida kubwa ya karoti mwilini ni kuboresha afya ya ngozi ya mtumiaji kwa sababu Vitamin A huboresha uwezo wa kuona lakini pia huyalinda macho kutonana na matatizo yanayotokana na uzee.

Karoti ni chanzo kizuri cha nyuzi nyuzi zenye virutubisho ambazo husaidia katika umeng’enyaji wa chakula na hivyo kurahisisha mtumiaji kupata haja kubwa kwa urahisi. Vile vile tunda hili hulikinga tumbo na magonjwa mbalimbali ikiwemo kuzua saratani ya utumbo na huimarisha afya ya kinywa kwani ulaji wa karoti hufanya kinywa kuwa chenye harufu nzuri lakini pia huimarisha fizi na kuzilinda zisishambuliwe na magonjwa ya kinywa. Karoti unaweza kuitengeneza juisi, saladi kwa kuchanganya na matunda, mbogmboga au kachumbari , lakini pia unaweza kuitumia kama kiungo katika mapishi yako.

Mbali na faida hizo, kiungo hiki kinapokuwa mwilini husaidia kusaga sumu zilizopo katika Ini na kuzisafisha katika kibofu na utumbo mkubwa ili ziweze kutolewa nje kwa njia ya haja ndogo au kubwa. Pia husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu kwani carotenoids iliyopo ndani ya karoti husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu.