http://www.swahilihub.com/image/view/-/4661218/medRes/2043554/-/j1ogofz/-/juliana.png

 

Juliana Yasoda kuzikwa Mpwapwa

Aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania, Juliana Yasoda  

Na Imani Makongoro

Imepakiwa - Friday, July 13  2018 at  13:52

Kwa Muhtasari

Alidondoka akiwa anapandisha ngazi kuelekea ofisini kwake

 

Dar es Salaam. Mwili wa aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania, Juliana Yasoda unatarajiwa kuzikwa Mpwampwa mkoani Dodoma.

Dada wa marehemu, Georgina Richard alisema msiba huko nyumbani kwa marehemu Kitunda Shule nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

"Tunamsubiri mtoto wa marehemu aliyeko China, atakapowasili Dar es Salaam ndipo taratibu za lini mpendwa wetu atapumzishwa katika nyumba yake ya milele zitapangwa kwa sasa mwili umeifadhiwa Muhimbili.

"Lakini kama familia tumepanga azikwe nyumbani Mpwampwa na kijana wake atakapowasili itapangwa tu ratiba ya mazishi," alisema Georgina.

Yasoda ambaye aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania kabla ya kuhamishiwa wizara ya elimu amefariki jana baada ya kudondoka akiwa anapandisha ngazi kuelekea ofisini kwake.

Hadi mauti yanamkuta Yasoda alikuwa Afisa idara ya sekondari katika wizara ya Elimu na aliiwakilisha wizara hiyo kwenye mashindano ya Copa Umisseta yaliyomalizika hivi karibuni jijini Mwanza.