Jumba alilonunua J Lo Marekani ni kufuru

Mwigizaji mahiri na mwanamuziki nyota duniani, Jennifer Lopez ‘J Lo’  

Imepakiwa - Friday, August 10  2018 at  15:22

Kwa Muhtasari

Lina uwanja wa ziada wa ekari nane

 

Los Angeles, Marekani. Mwigizaji mahiri na mwanamuziki nyota duniani, Jennifer Lopez ‘J Lo’, mwenye miaka 49, amenunua jumba lingine la kifahari eneo la Bel Air, Los Angeles, Marekani.

J Lo ambaye analo jumba kubwa, ameamua kuongeza jumba jingine jijini Los Angeles, ingawa anaendelea kusaka wateja wa kuinunua nyumba yake nyingine iliyopo eneo la California kwa Pauni 12.5 milioni.

Mwanamuziki huyu anayeingiza kipato kikubwa anaonekana kuchanganywa na kipato kwani jumba alilolinunua sasa lina uwanja wa ziada wa ekari nane, jumba hilo liliwekwa sokoni kwa Pauni 40 milioni lakini yeye alitoa ofa ya kununua kwa Pauni 28 milioni 

J Lo alilinunua jumba hilo mwaka 2010 akiwa na mumewe mwimbaji Marc Anthony kwa Pauni 8.2 milioni, awali aliiweka sokoni kwa Pauni 17 milioni, lakini ikakosa mteja.

Septemba mwaka huu J Lo aliamua kupunguza bei na kuiuza kwa Pauni 14.5 milioni hata hivyo hakuna mteja aliyepatikana hivyo sasa anaiuza kwa Pauni 12.5 milioni.