http://www.swahilihub.com/image/view/-/5056612/medRes/2298161/-/7h2y4oz/-/kangi+pic.jpg

 

Kangi Lugola naye kumenoga sasa?

Na  Mwandishi wetu

Imepakiwa - Thursday, April 4  2019 at  14:16

 

Dodoma. Namba moja alisema ‘rudini nyumbani kumenoga’ akiwapigia debe kampuni ya Mawasiliano ya Simu (TTCL) lakini jana Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akaibuka na rudini nyumbani kumenoga kwa aina yake.

Eti wanawake warudi nyumbani kumenoga na kuacha kushabikia watu wa nje, hee hata hayo mambo nayo kumenoga tofauti na nje. Vipi mura huyu!

Jana bwana wakati wabunge wanajadili maswali mjengoni, ilifika zamu ya mbunge Tauhida Cassian Gallos akauliza swali lake kuhusu raia wa kigeni ambao wanapewa vibali vya kufanya kazi nchini lakini wanawazalisha Watanzania na kuwaachia watoto.

Licha ya majibu mengi, si akaibuka Lugola na kuanza kuwapa darasa wanawake wa Kitanzania kuwa wasipende kuwashabikia wanaume wa kigeni kwani hata wanaume wa Tanzania wanafaa.

“Kwanza ni kosa kwa mujibu wa sheria kama mtu anazalisha mtoto halafu anamuacha, lakini humu bungeni kuna wakati watoto waliletwa na wakawa wanafana na watu Fulani. Kingine niwakumbushe wanawake wa Kitanzania warudi nyumbani kumenoga,” alisema.