http://www.swahilihub.com/image/view/-/5057796/medRes/2303236/-/13g9qpwz/-/unene+pic.jpg

 

Kimbiza unene na mlo sahihi

Na Mwandish wetu

Imepakiwa - Friday, April 5  2019 at  10:15

 

Tukizungumzia ugonjwa wa kisukari, hatuwezi kuacha kugusia chakula, mazoezi na unene. Vyakula tunavyokula hutengeneza nishati nayotumika kuupa nguvu mwili, kwa maana ya sukari na mafuta.

Vyakula hivi huupa mwili nguvu ya kufanya kazi na kila aina vya vyakula vina kazi yake katika mwili. Vyakula aina ya wanga huupa nguvu mwili kwa kuwa ni aina ya vyakula vinavyotengeneza sukari. Vyakula aina ya protini huukinga mwili na magonjwa mbalimbali, kuupa mwili kinga ya kupambana na magonjwa.

Mboga mboga na matunda ni kundi la vyakula lenye utajiri wa virutubisho, vitamini na madini na huboresha kinga ya mwili.

Unene ni moja kati ya sababu ya maradhi yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari, saratani, shinikizo la damu, maradhi ya moyo, tatizo la lehemu nyingi katika damu.

Pia, unene mkubwa kipindi cha ujauzito uweza kusababisha mimba kuharibika au kupata kisukari na shinikizo la damu.

Ulaji wa vyakula vya protini kama nyama, mayai, mafuta na wanga mwingi ni chanzo cha unene.

Unene wa mwili hufanya mwili usitumie sukari kama nishati na kuanza kutumia mafuta na kuacha sukari kuzagaa katika misuli bila matumizi na hali husababisha kisukari.

Mafuta mengi kwenye misuli na mashipa ya damu husababisha maradhi ya moyo na shikinizo la damu. Kwa watu wenye kisukari ni muhimu kupunguza unene wa mwili kwa kufanya yafuatayo.

Kupunguza kula vyakula vya wanga uliokobolewa na kupendelea kula wanga wenye asili ya nyuzinyuzi (dietary fibre) na mboga za majani kwa wingi katika kila mlo, vyakula vya protini asili ya mbegu mbegu kama maharagwe, choroko, kunde na mbaazi.

Aina hii ya protini kusaidia mwili kutoongezeka kwa sababu hazitengenezi mafuta.

Nyama nyekundu, mayai na maziwa halisi yana kiasi kikubwa cha mafuta ya lehemu (cholesterol) yasitumike kwa wingi. Mwandishi wa makala haya anaishi na kisukari, muelimishaji na mshauri lishe kwa wagonjwa wa kisukari