Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika shule za sekondari na elimu ya juu.

Imepakiwa - Monday, May 13  2019 at  09:22

 

Kwa muda mrefu, kumekuwapo na mjadala mrefu kuhusu
kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika
elimu ya sekondari na elimu ya juu. Kutokana na mijadala hii
mwaka 1976 Baraza la Kiswahili la Taifa liliamua kufanya utafiti
kuhusu hali halisi ya ufundishaji na ujifunzaji wa somo la
Kiswahili katika shule za sekondari. Maeneo muhimu
yaliyozingatiwa ni nafasi ya Kiswahili katika uchumi, sayansi na
teknolojia, afya , elimu, habari na mawasiliano na sheria.
Kiswahili katika shule za msingi:
Kiswahili ni lugha ya kufundishia katika shule za msingi na
Kiingereza somo la kawaida linalofundishwa kuanzia darasa la
111.
Kiswahili katika shule za Sekondari:
Kiswahili ni somo la kawaida ambapo Kiingereza ni lugha ya
kufundishia.
Kiingereza katika Elimu ya Juu:
Kiingereza ni lugha ya kufundishia katika elimu ya juu.
Mkanganyiko huu wa lugha wa kufundishia katika sera ya elimu
unaosababisha uelewa wa mdogo wa masomo hasa ya sayansi,
teknolojia na hisabati na hivyo unadunisha elimu yetu.
Mwaka ya 1976 Bazara la Kiswahili la Taifa (Bakita) liliona
mkanganyiko huu na likadhamiria kudhamini utafiti ili kupata
maoni ya walimu, wanafunzi na wadau wengine wa Kiswahili
hasa wananchi kwa jumla ili kupata maoni yao kuhusu matumizi

ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia n akujifunzia katika
shule za sekondari na elimu ya juu.
Wadau waliohusishwa ni walimu, wazazi, wanafunzi, viongozi
wa elimu katika ngazi za wilaya, mikoa nchi nzima pamoja na
Makao Makuu ya Wizara ya Elimu, Habari na Utamaduni
(wakati huo) wakiwamo wakurugenzi wa Mafunzo ya Ualimu,
Shule za Msingi na Sekondari na Ukaguzi wa Shule, Kamishna
wa Elimu, Katibu Mkuu na hatimaye Waziri wa Elimu
mwenyewe.
Watafiti walioshiriki ni Profesa Penina Mlama na Dk May
Matteru.
Jitihada za utafiti zilizofanywa:
Watafiti walitembelea shule, vyuo vya ualimu, ofisi za wakaguzi
wa elimu na viongozi wa elimu wilaya na mkioa. Wadau
walieleza kuwa suala la kukitumia Kiswahili kama lugha ya
kufundishia ni mwafaka lakini kunahitajika maandalizi na
jitihada kubwa na hasa sera ya elimu na kukaufaa yafuatayo:
a) Kutayarisha istilahi za kutosha za kuelezea dhana ngeni za
sayansi, hisabati, teknolojia, nk.
b) Kuwa na vitabu vya kufundishia (vya kiada, ziada)
c) Kuwa na walimu weledi (wazawa na wa kigeni) katika
lugha ya Kiswahili.
d) Kuwa na fedha za kutafsiri na kulipa mirabaha kwa
waandishi.
e) Kuwa na fedha za kulipia wachapishaji na waandishi wa
vitabu vitakavyotafsiriwa, kama malipo ya fidia.
Ratiba:

Watafiti waliandaa ratiba ya utekelezaji wakianzia masomo ya
sanaa na hatimaye masomo ya sayansi katika shule za
sekondari kwa kuanzia kidato cha 1 hadi cha VI.
Kuhusu elimu ya juu, utaratibu utakuwa kama ule wa shule za
sekondari wa kufuata hatua moja baada ya nyingime .
Katika Chuo Kikuu hatua ya kwanza ni kuanza na masomo ya:
i) Digrii za Sanaa
ii) Digrii za uchumi na Biashara
iii) Digrii za Sayansi- Elimu Mimea, Elimu Viumbe, Kemia,
Fizikia
iv) Hisabati
Masomo ya Sanaa:
Ilipendekezwa Kuanza na masomo ya sanaa kidato cha kwanza
hadi cha nne (kama historia, uraia, jiografia).
Baadaye masomo ya uchumi na biashara kidato cha 111 hadi
cha IV.
Masomo ya kidato cha tano na sita masomo ya sanaa.
Masomo ya Sayansi
Unaweza kuanza kufundisha kidato cha I hadi cha IV, masomo
ya kemia, elimu mimea, elimu viumbe na baadaye somo la
fizikia.
Vyuo vikuu vya Tiba, Uhandisi, Teknolojia, Elimu Udongo na
Miamba, nk. wawe tayari kujiandaa kwa mageuzi haya.
Bakita, Taasisi ya Elimu Tanzania na Baraza la Mitihani
wanashauriwa kuandaa ratiba ya utekelezaji kwa kshirikiana.
Muda wa Utekelezaji:
Kuwe na kipindi cha maandalizi kwa walimu walio kazini na pia
wakurufunzi walio vyuoni.
Pili, vitabu vianze kuandaliwa. Njia zifuatazo znaweza kutumika
kwa:
i) Kuandaa miswada ya vitabu vya kuchapisha
ii) Kuichapisha miswada hiyo kuwa vitabu
iii) Kusambaza vitabu shuleni na vyuoni
iv) Kuwaandaa walimu kwa kutayarisha warsha za
kuwapiga msasa
a) Muda wa kuandaa vitabu uweKuandaa tariban miaka
miwili
b) Muda wa kuwaandaa walimu na wakufurunzi uwe ni
mwaka mmoja
Suala la msingi ni kwa Bakita kuandaa istilahi za masomo
yote ili iwe rahisi kutumia istilahi hizo kwa akijli ya kutafsiri
na kuandika vitabu, matini na makala za kitaaluma.
Vyombo vya habari navyo vitumike kuielimisha jamii kuhusu
hali hii ili wananchi wawe na uelewa wa kutosha.

Viongozi wa Serikali nao wawe na utashi wa kisiasa kwa
kusukuma mbele azma hii. Pia Serikali iwe tayari kuandaa sera
ya lugha ya Kiswahili na kuiweka wazi kwenye Katiba Mpya.
Kama hatua hizi zitazingatiwa, suala la Kiswahili kuwa ni lugha
ya kufundishia na kujifunzia katika elimu zitaweza kufanikiwa.