http://www.swahilihub.com/image/view/-/4706576/medRes/2075120/-/dc3wkcz/-/enald.jpg

 

Lindi watahadharishwa uwezekano wa kuongezeka maambukizi ya VVU

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Dk Leonard Maboko  

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Friday, August 10  2018 at  12:43

Kwa Muhtasari

Kutoa elimu ya kujikinga na mabadiliko ya tabia

 

Lindi: Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Dk Leonard Maboko amesema matokeo ya utafiti wa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) mwaka 2016/17 yanaonyesha kuwa maambukizi mkoani hapa ni asilimia 0.3 huku kiwango cha kitaifa ni asilimia 4.7.

Alitoa kauli hiyo baada ya kutembelea mkoani hapa kufanya tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za Ukimwi zinavyotekelezwa.

Dk Maboko pia alikutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi.

Alisema matokeo ya utafiti huo kwa Lindi hauna maana kuwa maambukizi hayawezi kuongezeka, bali kinachopaswa kufanyika ni kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi pamoja na elimu ya mabadiliko ya tabia.

Mkuu wa mkoa, Zambi alisema elimu kuhusu maambukizi hayo inatolewa kwa kuwa uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi haupingiki. Zambi alizungumzia fursa zilizopo mkoani hapa akisema kwa sasa wawekezaji wanaanza kujitokeza katika sekta ya madini japo bado wapo katika hatua za awali za uwekezaji, pia kuna ongezeko la viwanda na shughuli nyingine za uvuvi.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Lindi, Emmanuel Lwero alisema wanaendelea kutoa elimu ya kuzuia maambukizi mapya ya VVU kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Alisema wameweza kudhibiti baadhi ya tabia hatarishi hasa kupunguza athari zitokanazo na mila na desturi zilizopitwa na wakati zinazosababisha maambukizi ya VVU.