Maadili katika uandishi

Na  Stephen Maina

Imepakiwa - Thursday, May 9  2019 at  12:41

 

Yako maeneo matatu niliyogusa nilipoandika
katika makala zangu ambayo yametiliwa mkazo
katika kitabu cha Mwongozo kwa Wanahabari
katika vyombo vya habari. Maeneo haya
yanahusu matumizi ya maneno
yanayokanganya, miundo isiyokubalika na
tahijia mbovu inayosababishwa na matumizi ya
maneno ya kilugha/asili yanayoathiri pia
matamshi ya maneno sanifu.
Nimewalenga wanahabari wanaowaandikia
wanajamii wanaowazunguka na ambao wako
chini ya usimamizi ya Kampuni ya Nation Media
Group. Katika kampuni hizi ziko kampuni tanzu
zinazojishughulisha na uandishi na uchapishaji
wa magazeti kama kampuni tanzu ya
Mwananchi Communications Limited (MCL)
inayochapisha magazeti ya Kiswahili ya
Mwananchi na Mwanaspoti.

Kwa upande wa Kenya liko gazeti la Taifa Leo na
Taifa Jumapili. Magazeti haya yanaandikwa kwa
Kiswahili na juhudi hizi zilianza tangu mwaka
1959. Katika upande wa redio, iko redio moja
chini ya NMG ambayo inatangaza kwa Kiswahili
nayo ni QFM. Kwa upande wa runinga, ziko
runinga mbili mashuhuri ambazo ni QTV na
NTV. Runinga ya QTV ina programu nyingi za
Kiswahili zilizo chini ya himaya ya NMG.
Kwa bahati mbaya nchini Uganda iko runinga
moja na gazeti moja yote yakiwa chini ya NMG.
Gazeti hilo na runinga hiyo vyote vinaandikwa
kwa Kiingereza. Kama vyombo hivi vingekuwa
vinatumia lugha ya Kiswahili nina hakika
kwamba Kiswahili kingepiga hatua kubwa katika
kuielezea jamii ya Waganda katika masuala ya
uchumi, utamaduni, elimu teknplojia na siasa.
Wako Waganda ambao wanafahamu Kiswahili
na ni wale waishio jijini Kampala. Katika kambi
za majeshi ya ulinzi na usalama, Kiswahili
kilitumika kama lugha ya mawasiliano wakati

wa enzi ya Kiongozi Idd Amin Dada. Baada ya
hapo haipo sera ya lugha inayogusia ukuzaji na
uendelezaji wa Kiswahili.
Ijapokuwa Tanzania inajivunia kuwa ni kitovu
cha Kiswahili, bado kuna kazi kubwa ya kufanya
kukiimarisha Kiswahili kama lugha ya
mawasiliano kwa wananchi wa kawaida waishio
mpakani mwa nchi za Kenya na Tanzania.
Wananchi hawa ni wa pande zote mbili na
wanajishughulisha na mambo mbalimbali ya
kiuchumi kama uvuvi, kilimo na biashara ndogo
ndogo za ujasiriamali. Matumizi ya lugha ya
mawasiliano inayokubalika ni Kiswahili.
Majirani zetu hawa ni Waganda, Warundi,
Wanyaruanda na Wakongo.

Katika kuimarisha uelewa wa lugha mpakani,
vyombo vya habari kama redio na runinga
inafaa kuzingatia makubaliano yaliyofikiwa kati
ya viongozi wetu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki lugha ya kutumia lugha ya Kiswahili

kama lugha ya mawasiliano kwa jamii yote.
Lugha hii inatakiwa iwe rahisi kwa maana ya
kutumia maneno ya rahisi na ya kawaida na
miundo ya sentensi iwe fupi.
Nitoe mifano michache ya kile kinachosikika
kutoka kwa watangazaji. Hawa wanakipotosha
Kiswahili kwa kuchanganya maneno ya Kiswahili
na ya Kiingereza. Wanatangaza kama vile wako
kwenye semina au kongamano lenye hadhira ya
wasomi. Kwa mfano, mtangazaji mmoja
alisema:
a) Nafikiri this time masuala ya utaifa
yanatakiwa kuwekwa mbele.
b) Unajua sometimes tujiweke sawa.
c) Nadhani the best way kwa Watanzania
kufikia mafanikio ni kufanya kazi kwa bidii.
d) If you are trying to hide something
watakukamata tu.
e)Jana ilikuwa bombastic, kwa hiyo mambo
yalikuwa poa tu.

Iko mifano mingi ambao naweza kuitoa lakini
hiyo hapo juu inatosha.
Msikilizaji wa kawaida anaposikia lugha ya
aina hii anakichukia Kiswahili kwani haelewi
baadhi ya maneno. Hata hivyo anapata faraja
anaposikia kwa mfano”
a) Nafikiri masuala ya utaifa yanatakiwa
kuwekwa mbele.
b) Unajua wakati mwingine tujiweke sawa.
c) Nadhani njia bora kwa wananchi kufikia
mafanikio ni kufanya kazi kwa bidii.
d) Kama unajibu kuficha kitu
watakukamata tu.
e) Jana mambo yalikuwa safi sana.
Nigusie kidogo kuhusu waandishi wa michezo.
Hawa wana changamoto kubwa katika
matumizi ya Kiswahili sanifu kwani
wanapambana na misamiati na istilahi ngeni
ambazo hazijapatiwa tafsiri sanifu.

Kwa mfano mwandishi mmoja aliandika:
“Wakati wa maandalizi ndiyo sasa ili itakapofika
Septemba mwakani wawe wako tayari kwa
mashindano ili aibu iliyotokea kwenye Madola
isijirudie kwenye All African Games huko
Brazaville, Kongo.”
Kama mwandishi hapati tafsiri ya msamiati au
istilahi sanifu asihofu kwani anaweza kutumia
alama za mnukuo kwa maneno yasiyokuwa na
tafsiri sanifu. Kwa mfano tunaweza kuandika,
“All African Games” na inatosha.
Mwisho
O754 861664
stephenjmaina@tz.nationmedia.com