http://www.swahilihub.com/image/view/-/4844334/medRes/2165399/-/sc1jfe/-/wavuvi.jpg

 

Mali za wavuzi haramu zataifishwa

Wavuvi wakiwa kwenye mitumbwi huku wakiandaa nyavu kwa ajili ya kuvulia samaki  

Na Johari Shani, Mwananchi

Imepakiwa - Friday, November 9  2018 at  14:54

Kwa Muhtasari

Wavuvi hao watalazimika kulipa faini ya Sh2 milioni kila mmoja

 

 

Mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Rorya. Wavuvi 21 wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kujihusisha na uvuvi haramu. Mitumbwi minane na injini zake zitataifishwa na Serikali baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Licha ya kutaifisha mali hizo, wavuvi hao watalazimika kulipa faini ya Sh2 milioni kila mmoja kuepuka kufikishwa mahakamani na pengine kufungwa jela iwapo watatiwa hatiani.

Wakati wavuvi 15 raia wa Tanzania wataachiwa huru baada ya kulipa faini, wenzao sita raia wa nchi jirani ya Kenya ambao pia wanashikiliwa watakabidhiwa kwa Idara ya Uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume na sheria.

Ofisa mfawidhi ulinzi wa rasilimali za uvuvi Kanda ya Ziwa Victoria, Didas Mtambalike alisema wavuvi hao walitiwa mbaroni Novemba 6 kijiji cha Bubombi wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Alitaja baadhi ya tuhuma dhidi ya wavuvi hao kuwa ni kutumia nyavu haramu za dagaa za milimita sita, kuvua bila leseni, kutojisajili na kutumia taa za nishati ya jua (solar) zisizoruhusiwa.

Kuhusu ziara ya maofisa uvuvi wilayani Rorya, mwenyekiti wa kijiji cha Sota, Ramadhan Said aliwasihi wavuvi raia wa Tanzania kulinda rasilimali ya samaki na mazao yake kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.