Mama aieleza korti jinsi mtoto wake alivyolawitiwa

Na Pamela Chilongola, Mwananchi

Imepakiwa - Friday, January 11  2019 at  09:18

Kwa Muhtasari

Nilipewa fomu ya PF3 ya kwenda katika zahanati ili mtoto aweze kutibiwa

 

pchilongola@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mama ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam jinsi mtoto wa miaka saba alivyolawitiwa na jirani yake (38) jina linahifadhiwa.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda shambulio hilo la aibu Julai 24 mwaka jana maeneo ya Kimara Stop Over kwa kumwingizia uume mdomoni na kwenye haja kubwa mtoto wa kiume wa miaka saba.

Mama wa mtoto huyo jana aliieleza Mahakama siku hiyo saa 10:00 jioni mwanaye alipotoka shuleni aliishia nje ya geti na alipomuita aingie ndani alikataa.

Alidai alipotoka nje hakumkuta mwanaye, alielezwa na fundi aliyekuwa akijenga nyumba ya jirani kuwa aliitwa na jirani yake.

Mama huyo alidai mshtakiwa alimpeleka mwanae kwenye nyumba ambayo haijaisha na kumvua kaptula na kuanza kumwingiza uume wake kwenye njia ya haja kubwa.

Alidai kutokana na mtoto huyo kupata maumivu makali, mshtakiwa alimpaka mate sehemu ya njia ya haja kubwa na kuingiza tena uume wake.

Mama huyo alidai baada ya mtoto huyo kuendelea kupata maumivu makali mshtakiwa alihamisha uume wake na kumweka kwenye mdomo.

“Baada ya kuelezwa hayo na mwanangu nilienda nyumbani kwa mtuhumiwa lakini sikumkuta nikaenda kituo kidogo cha polisi cha Kimara nikapewa fomu ya PF3 ya kwenda katika zahanati ili mtoto aweze kutibiwa,” alidai mama huyo.

Mahakama hiyo imepokea kielelezo namba moja fomu ya polisi kwa ajili ya matibabu (PF3) kutumika kwenye ushahidi.