http://www.swahilihub.com/image/view/-/5065022/medRes/2308485/-/mo0ei4z/-/shaban+pic.jpg

 

Mapenzi Bora

Na Shaaban Robert

Imepakiwa - Wednesday, April 10  2019 at  11:55

 

Hiki ni kitabu chenye mashairi mengi na beti zisizopungua 690. Kitabu hiki kiliandikwa na Marehemu Shaaban Robert mwaka 1958.

Shaaban Robert ni nguli wa lugha ya Kiswahili na amebobea hasa katika upande wa fasihi. Akieleza kusudi la kuandika kitabu hiki alisema, “kuandalia mahitaji ya watu waliofikia fahamu ya kuwaza na kuhoji neno au kitu au tendo kwa akili”. 

Watu ambao wana dhana ya kuwa mapenzi si kitu cha maana, wanaonywa katika kurasa hizi kuwa wanapatwa na hasara kubwa. Baadhi ya watu hudai kuwa mapenzi ni karaha kuzungumzwa. Yafaa watu waelewe kuwa Kiswahili si lugha ya watoto na vitabu vya chuoni tu. Huweza kuzungumza biashara, dini, sheria na mapenzi.

Wale wasemao kwamba mapenzi ni karaha hawawafunzi wazazi kukaa vyema na watoto  wao wala watoto kuwa wema na amani kwa wazazi wao. Hawawafunzi watu kuwa na wajibu wa kutegemeana katika dunia. Huharibu umoja na ujirani, uaminifu na urafiki.

“Mapenzi ni moja ya mambo yaliyo muhimu na wajibu kwa mtu katika maisha yake,”alisisitiza.

Katika tenzi alizoandika Shaaban Robert kuhusu “Mapenzi Bora”, anaanza utenzi wake kama ifuatavyo:

1.Jina limetakadimu,

    Na moyo umeazimu,

    Kabla juma kutimu,

    Kuandika simulizi.

 

2.Pindi nikiwa mzima,

Muda ukipita juma

Tawapa habari nzima,

Nikijaliwa pumzi.

 

3.   Nikifunguliwa heri,

 Na nguvu ya kufikiri,

Nitatunga kwa shairi,

Wimbo tunu nchi hizi.

 

4. Hata kama siku hizi

Mwili wangu una ganzi,

Kabla robo  ya mwezi,

Makala yatabarizi.

 

5. Yatabarizi makala,

Kwa uwezo wake Allah,

Apaye watu chakula

Uzima na usingizi

 

6.Toka kalamu kushika,

Arobaini miaka,

Bado sijapumzika,

Na kuiacha siwezi.

 

7.Kutunga na kutangua

Kuwaza na kushangaa,

Sijakoma robo saa,

Kila siku nina kazi.

 

8. Kwa wino na kalamu,

kusoma na kudurusu,

Macho yangu nayahisi,

Kuona yana tanzu.

 

9. Kuona natatizika,

Kwa nuru kunitoweka,

Na kila nikiandika,

Herufi si wazi.