http://www.swahilihub.com/image/view/-/4798710/medRes/2135851/-/404e29z/-/kent.jpg

 

Masomo na ufadhili

Chuo Kikuu cha Kent  

Na Elizabeth Edward

Imepakiwa - Tuesday, October 9  2018 at  17:20

Kwa Muhtasari

Umahiri katika lugha ya kiingereza ni kigezo muhimu kitakachozingatiwa

 

Chuo Kikuu cha Kent kilichopo Uingereza kinatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na shahada ya kwanza.

Ufadhili huu unatolewa katika School of Anthropology & Conservation na unawalenga wanaotaka kujiunga na shahada ya kwanza na ya pili.

Vigezo: Umahiri katika lugha ya kiingereza ni kigezo muhimu kitakachozingatiwa. Mwombaji anatakiwa awe na uzoefu katika masuala ya uhifadhi.

Mwisho wa maombi: Aprili 16, 2019. Tuma maombi:https://www.kent.ac.uk

Taasisi ya OFID inatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa mataifa yote yanayoendelea kwa ajili ya kujiunga na shahada ya uzamili.

Ufadhili huu kwa ni ajili ya wale wanaotaka kusoma masuala yahusuyo maendeleo ya jamii ikihusisha kukabiliana na umaskini, nishati na kuzuia uharibifu wa mazingira.

Ufadhili unatolewa katika vyuo vyote vilivyothibitishwa na taasisi za elimu za nchi husika. Taasisi itahusika katika kulipia gharama zote za masomo .

Atakayepata ufadhili huu atalipiwa pia bima ya afya, gharama za usafiri na fedha za kujikimu kila mwezi kwa mwaka mzima.

Vigezo: Mwombaji anatakiwa awe na umri kati ya miaka 23-32

Mwombaji lazima awe amepata shahada ya kwanza kutoka katika chuo kinachotambulika. Lazima awe amefaulu kwa GPA kuanzia 3 na kuendelea. Ni lazima mwombaji awe anatoka kwenye taifa linaloendelea

Mwisho wa maombi: Mei 4, 2019. Tuma maombi:http://www.ofid.org

Taasisi ya ESMT Berlin inapokea maombi ya ufadhili kwa wanafunzi wa kike wanaotaka kujiendeleza kimasomo katika kozi ya teknolojia ya habari.

Ufadhili huu utawahusu sana wataaam wa IT ambao tayari wameshafanya kazi kwenye taaluma hiyo na wanataka kuongeza ujuzi.

Milango imefunguliwa kwa wale wanaotaka kujiunga na shahada ya uzamili.

Ufadhili huu utatolewa nchini Ujerumani katika vyuo mbalimbali vinavyotoa kozi zinazohusiana na masuala ya IT.

Mwombaji atalipiwa asilimia 50 tu ya ada, kiasi kinachosalia kinatakiwa kuchangiwa na mwanafunzi bila kusahau gharama nyingine katika kipindi chote atkachokuwa chuoni.

Mwisho wa maombi: Machi 30, 2019. Tuma maombi:http://scholarship-positions.com

Chuo kikuu cha Sydney kilichopo Australia kinatoa nafasi za ufadhili kwa wanaotaka kujiendeleza na shahada ya uzamili na uzamivu.

Vigezo: Lugha ya kiingereza ni kigezo muhimu kwa waombaji.  Waombaji wenye ufaulu mkubwa watapewa kipaumbele.

Mwombaji anatakiwa aandike insha ya maneno 1000 akieleza kwanini apewe ufadhili huo.

Mwisho wa maombi: Machi 2018. Tuma maombi: http://sydney.edu.au

Taasisi ya Emile Boutmy inatoa nafasi za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kutoka mataifa yanayoendelea wanaotaka kujiendeleza katika masomo ya sayansi.

Ufadhili huu unatolewa katika Chuo kikuu cha Sciences Po kilichopo Paris Ufaransa na unalenga kuwanufaisha wanafunzi kwa ngazi ya shahada ya kwanza na uzamili. Ufadhili utahusisha kozi zote zinazotolewa chuoni hapo.

Vigezo: Mwombaji hatakiwi kuwa na uraia wa nchi yoyote kutoka Umoja wa Ulaya, wala asiye ambaye amewahi kusoma katika nchi hizo.

Waombaji wenye ufaulu mzuri watapewa kipaumbele. Umahiri wa lugha ya kiingerea ni muhimu kwa kila mwombaji

Mwisho: Aprili 26, 2019. Tuma maombi:.http://www.sciencespo.fr