http://www.swahilihub.com/image/view/-/4885332/medRes/2191362/-/lq7w1/-/mazoezi.jpg

 

Mazoezi ya kukupa mwonekano mzuri wa mwili

Mtu akifanya mazoezi ya kumpa mwonekano mzuri wa mwili   

Na Herieth Makwetta, Mwananchi

Imepakiwa - Friday, December 7  2018 at  11:03

Kwa Muhtasari

Fanya mazoezi kwa dakika zisizopungua 30 angalau mara 3 mpaka tano kwa wiki

 

hmakweta@mwananchi.co.tz

Kama unataka mwili wa kuvutia au kuwa na mwonekano mzuri, kuna mengi yanayotakiwa kuzingatiwa kuanzia unachokula na namna unavyoutunza mwili wako.

Mtaalamu wa mazoezi ya afya na mkufunzi kutoka Chuo cha American Sports Medicine ACSM, Dk Waziri Ndonde anaelezea aina ya mazoezi ambayo yatauacha mwili wako kuwa na mwonekano wa kuvutia.

Kuna aina tatu za mazoezi

Mazoezi yakupunguza mwili; mfano kutembea, kuogelea, kuendesha baiskeli, kucheza muziki na kukimbia mchakamchaka.

Mazoezi ya kuimarisha misuli na mifupa; kama vile kupiga pushapu, kujivuta juu, kuimarisha misuli ya tumbo.

Mazoezi ya kukunja viungo. Mfano wa mazoezi haya ni yale yanayosaidia kuuvuta mwili, misuli na viungio kufanya kazi.

Umbo zuri ni lipi?

Kuwa na afya bora ina uhusiano mkubwa wa kuwa na umbo zuri, binadamu anatafsiriwa kuwa ana umbo zuri ni pale anapokuwa na muonekano mzuri uliojengeka kiafya.

Kuna vipengele vitano muhimu kwenye afya ya mazoezi ambayo inamtafsiri binadamu mwenye umbo bora na zuri.

Kuwa na uwezo mkubwa wa mapafu na moyo kufanya kazi. Misuli ya moyo inapaswa kuwa imara ili iweze kusukuma damu vizuri.

Uwezo wa misuli kuwa imara na kufanya kazi. Tunatafsiri muonekano bora wa mtu kwa kuangalia ubora wa misuli yake imara.

Kuweza kuikunja; umbo bora ni lile ambalo viungio vyake ni vyepesi kujikunja.

Uwiano wa kiwango cha mafuta kwenye misuli yake.

Jambo la mwisho ni lishe; ili uweze kuwa na mwili ulio na muonekano bora unahitaji ule mlo ulio kamili; mlo unaojumuisha makundi matano ya vyakula ambavyo ni wanga, mboga, matunda, mafuta na mazao ya wanyama.

Kiwango cha asilimia ya mafuta kwenye mwili

Mazoezi

Kwanza jipime urefu wako kwa rula, angalia una sentimita ngapi, kisha toa 100 utakacho bakia nacho ndio uzito wako sahihi. Mfano; mtu mwenye 168cm akitoa 100 anabakiwa na 68 (huu ndio uzito wako stahiki).

Kwa hiyo hatua ya kwanza ya kutafuta umbo zuri ni kuhakikisha kama uzito wako umezidi, hapo lazima ufanye mazoezi ya kupunguza uzito:

Fanya mazoezi kwa dakika zisizopungua 30 angalau mara 3 mpaka tano kwa wiki.

Mpangalio wa mazoezi

Siku ya kwanza fanya mazoezi ya kupunguza uzito na jumuisha na mazoezi ya kuimarisha misuli ya juu, kifua, mikono na mabega

Siku ya pili; fanya mazoezi ya kupunguza uzito kwa dakika 30, fanya mazoezi ya kuimarisha misuli ya mgongo na tumbo

Siku ya tatu; fanya mazoezi ya kupunguza mwili kwa dakika 30; fanya mazoezi kuimarisha misuli ya miguu

Zingatio

Jitahidi zoezi lako liwe zito zaidi muda wote unapofanya. Kunywa maji mara kwa mara unapfanya mazoezi na baada ya kufanya mazoezi.

Usipende kufanya mazoezi muda mrefu sana kwani utaufanya mwili uchoke na kupata maumivu

Tambua kuwa zao bora la zoezi linapatikana unapokuwa na muda wa kupumzika na kupata lishe bora.