http://www.swahilihub.com/image/view/-/4885274/medRes/2191309/-/lfxnux/-/upofu.jpg

 

Mwenye Kisukari anavyoweza kuepuka upofu

Macho yaliyoharibika kwa upofu kutokana na ugonjwa wa kisukari 

Na Lucy John Bosco

Imepakiwa - Friday, December 7  2018 at  10:41

Kwa Muhtasari

Ugonjwa wa kisukari unachangia asimilia 10 ya upofu duniani

 

Wagonjwa wa kisukari wapo katika hatari kubwa ya kupata upofu mara mbili zaidi ya watu wasio na ugonjwa wa kisukari.

Hii ni ikiwa watashindwa kudhibiti kiwango cha sukari. Wizara ya Afya imewahi kuthibitisha kuwa kisukari kinasababisha upofu kwa asilimia 4.8 ya wagonjwa wote nchini.

Upofu huu unaosababishwa na kisukari ni tatizo kubwa sana hujulikana kitaalamu kama ‘Diabetes Retinopathy.’

Diabetes Retinopaty ni tatizo la macho linatotokana ana kiwango cha sukari kuwa juu sana; huathiri vimishipa vidogo vilivyo nyuma ya pazia ya jicho.

Mishipa hii huziba na kufanya damu isifike katika sehemu ya retina na mwisho wake mishipa hii hupasuka na kuvuja damu mpaka sehemu ya mbele ya jicho au retina.

Mgonjwa asipowahi kufika katika kituo cha afya mapema hali hii inaweza kusababisha upofu. Lakini pia kuna maradhi mengine ya macho yanayosababishwa na ugonjwa wa Kisukari Maradhi haya ni pamoja na ugonjwa wa mtoto wa jicho. Sukari ikiwa juu sana husababisha mtoto wa jicho. Mgonjwa anaweza kujua kuwa amepata tatizo la mtoto wa jicho kwa kuona dalili zifuatazo:

Macho kupata ukungu katika lenzi ya jicho, kuona moshi mbele yako na kushindwa kuona vizuri na pengine mboni ya jicho kuwa na weupe weupe. Mgonjwa akiona dalili hizi ni muhimu aende katika kituo cha afya na pia kuanza kudhibiti kiwango cha sukari. Presha ya jicho ni tatizo jingine ambalo husababishwa na ugonjwa wa Kisukari. Watalaam wanasema kuwa mgonjwa wa kisukari yupo katika hatari kubwa ya kupata tatizo la presha ya macho. Tatizo hili linachangia asimilia 10 ya upofu duniani. Ugonjwa huu pia unakuwa na viashiria vyake lakini viashiria hivi vinajitokeza baadaye, kwa maana kuwa hakuna dalili za mwanzo za ugonjwa huu.

Mgonjwa wa kisukari akianza kupata dalili zote zilizotajwa hapo juu, asianze kuhangaika kutumia dawa za macho tofauti tofauti, kwani anaweza kuongeza tatizo. Aende katika kituo cha afya na kufanya vipimo vya macho na sukari

Mgonjwa wa Kisukari anaweza pia kuwa na upungufu wa vitamin kama vitamin A, ambayo husababisha pia matatizo ya macho kwa kuleta vidonda kwenye kioo cha jicho.

Mgonjwa wa kisukari akianza kupata dalili zote zilizotajwa hapo juu, asianze kuhangaika kutumia dawa za macho tofauti tofauti, kwani anaweza kuongeza tatizo. Aende katika kituo cha afya na kufanya vipimo vya macho na sukari.

Wagonjwa wa kisukari wenye umri wa miaka ya 40 na hasa wenye aina ya pili ya kisukari, ni muhimu kupima macho yao angalau mara moja kila mwaka.

Mgonjwa wa Kisukari lazima ajue historia ya maradhi ya macho katika familia, kuhakikisha kiwango cha sukari kinakuwa sawa, kula mboga za majani kwa wingi na matunda na kuacha kutumia dawa za macho bila kufanya vipimo.