NYIMBO ZA HAJI GHORA

Imepakiwa - Wednesday, April 10  2019 at  12:01

 

Kisiwani  Tumbatu kulikuwa na matukio mengi ya nyimbo kama vile harusi, ngomani,

 kumlaza mtoto, nk. Sifa za nyimbo hizo ni kwa ajili ya kuchombezea watoto. Nyimbo

 chache anazozikumbuka ni:

a) Kazija mwenzako kaja

Tuje sema kwa umoja

Umja wa mwanandani

Mwanandani mtu mwema

Huenda akaswalai Jumwa

Na vipindi vema vyema

 

b) Owa mtoto owa

    Tumchuchile alale

Mame kende chokoa

Kende chokoa mayale

Mayale ya mwanandani

Mwanadani mtu mwema

Kendee Kuswali Jumwa

 Na vipindi vyema vyema

Owa mtoto owa

Owa mtoto owa.

 

Ubwabwa wa mtoto hali mamie

Ubwabwa wa mtoto hali babie

Ubwabwa wa mtot hali dadiye,

Ubwabwa wa mtoto hali kakiye

 

Ubwabwa wa mtot hali bauye

Owa mtoto owa

Owa mtoto owa

TAARAB

Baada ya kuona kuwa kipaji chake kimefikia kileleni na hakuna nafasi ya kujiendeleza,

aliamua kuhamia mjini . Alipata nafasi ya kujiunga na kikundi maarufu cha Michenzani

Social Club kilichokuwa na taarab na michezo ya maigizo.

Shairi lake la kwanza lilikuwa la Dunia Rangi Mbili lilitiwa sauti na kuimbwa na Khamis Abeid

 Shairi lilsema:

Dunia ni rangi mbili, hilo nalikumbukia,

Wema ndio wa awali, ya pili ubaya

Dunia ni kitu dhakili, mara kuhugeukia

 

Asali hukurambisha hadhi kukuondokeya

Watu hukufurahisha usemalo huwa baya,

Yako huyakamilisha kila unokusudiya

 

Jivuli likikupita, hadhi hukuondoleya

Kila mmoja huguta, na watu kukukimbiya

Utaliya na kujuta, ikikutenga dunia.

 

Si kama kitendewili, kutega nakusudiya,

Kwa wengi yamekabili, kama hayo kutokeya

Dunia kiwwabadili mauti hujiombeya