Ndugai tegua kitendawili bwana!

Na  Mmwandishi wetu

Imepakiwa - Thursday, April 4  2019 at  14:30

 

Dodoma. Mheshimiwa Spika kwani walikuwa wanatajwa humu ndani kabla ya kauli yako, au uliamua kusema ili wasitaje kitu kingine. Nilikusikia jana ukitetea chombo chako kitukufu cha kutunga sheria kwamba hakuna hata mmoja ambaye anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Ni Spika Job Ndugai ambaye jana katika mkutano unaoendelea alikuwa anaongoza kikao bungeni lakini katika pitapita ya maswali, likaibuka swali la Nagma Giga kuhusu masuala ya ushoga.

Mgogo akaona isiwe tabu maana ukimya mwingi huzaa mshangao ambao mwisho wake watu wanajenga hisia ya mambo potofo akasema: “Humu bungeni hakuna kabisa masuala ya mapenzi ya jinsia moja.”

Sasa kilichoshangaza ni baada ya kauli ya Spika kelele zikasikika kutoka kwa wabunge kuwa haaa, akasisitiza tena kuwa hakuna watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja mjengoni.

Dah, sijui aulizwe nani katika jambo kama hili maana kiongozi anasema halafu watu wanapiga kelele sasa walitaka kusema nini?