http://www.swahilihub.com/image/view/-/4799420/medRes/2006828/-/jpqabez/-/rembo.jpg

 

Njia sahihi ya kung’arisha ngozi yako

Mrembo akijiangalia kwenye kioo  

Na Pauline Ongali

Imepakiwa - Wednesday, October 10  2018 at  09:38

Kwa Muhtasari

Usinawe uso wako kupita kiasi kwani huenda ukaondoa mafuta muhimu

 

Ni wazi hakuna changamoto inayowakumba wanawake kama kuwa na ngozi angavu.

Wengi huishia kutumia bidhaa ghali na wakati mwingine hatari. Hata hivyo, mbinu hizi za kawaida zitahakikisha kuwa unaafikia hili.

Nawa uso: Kila mara nawa uso wako kabla ya kwenda kulala. Hii ni mbinu mwafaka ya kuondoa uchafu na mafuta ambayo yamejikusanya kwenye ngozi wakati wa mchana.

Iwapo hautafanya hivyo, basi unaweza ukasababisha vinyweleo vya ngozi kuziba na kusababisha chunusi. Kadhalika unashauriwa kunawa uso asubuhi kutokana na kuwa bidhaa za nywele na ngozi hufyonzwa kwenye vinyweleo vya ngozi unapolala na zaweza ziba vinyweleo na kusababisha chunusi.

Lakini hata unapozidi kufanya hivyo kuwa mwangalifu usinawe uso wako kupita kiasi kwani huenda ukaondoa mafuta muhimu ya ngozi. Badala yake tumia cleanser kila unapohisi kana kwamba ngozi yako imejaa mafuta.

Tumia cleanser: Hii ni mbinu ya kuondoa kabisa uchafu uliojikusanya kwenye ngozi.

Lakini unapofanya hivyo hakikisha unasuuza cleanser yote kwani mabaki yake kwenye ngozi husalia na kuwa uchafu.

Kusugua taratibu: Usiwe na mazoea ya kusugua ngozi kwa nguvu kwani hii husababisha ngozi kukwaruza na hata kwa watu wengine kubadili rangi na kuwa nyekundu.

Usitumie scrub zenye kemikali kali au hata vitambaa vigumu. Badala yake nawa uso kwa kutumia mikono yako.

Exfoliate: Hii inasaidia kuondoa safuza ngozi iliyokauka na uchafu ambavyo huziba vinyweleo na kusababisha chunusi.