http://www.swahilihub.com/image/view/-/4878794/medRes/2187249/-/jd8rs3/-/lipsiki.jpg

 

Njia za kufanya midomo kuwa laini

Midomo laini

Midomo laini. Picha/MAKTABA 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Monday, December 3  2018 at  10:32

Kwa Muhtasari

Ni muhimu kuitunza midomo yako ili iwe laini na ya kupendeza.

 

WATU wengi hasa wanawake wanapenda kuwa na midomo laini. Hata hivyo, wengi hujikuta katika hali tofauti kabisa ambapo midomo yao hubakia imekauka kama kuni.

Kwa kiwango fulani, asili ya mtu na hali ya hewa, vimechangia pakubwa kwa mtu kuwa na midomo migumu isiyovutia hata kidogo. Kama wewe ni mwathirika wa tatizo hili unaweza kufanya vifuatavyo:

Kunywa maji mengi

Ukosefu wa maji mwilini si mzuri kwa afya ya ngozi yako. Njia nzuri ya kukuza afya ya ngozi yako ni kwa kunywa maji mengi kila siku. Hii itakusaidia kuboresha ngozi yako, kukuza seli mpya na kuweka ngozi yako hali ya unyevu

Sugua midomo kwa kutumia vipande vya tango

Kusugua midomo yako kwa kutumia vipande vya tango husaidia kulainisha na kuzing’arisha lips zako. Matango yana kemikali ya asili aina ya phytochemicals ambayo itasaidia kulainisha midomo yako pamoja na kuifanya iwe na unyevu.

Tumia mafuta ya nazi

Mafuta ya nazi yana matokeo mazuri sana katika ngozi ya mwanadamu. Paka kiasi kidogo tu cha mafuta ya nazi kwenye midomo yako. Mafuta haya husaidia kulainisha na kuiweka midomo yako katika hali ya kuvutia.

Paka mafuta ya petroleum jelly kabla ya kwenda kulala

Kupaka mafuta muda mfupi kabla ya kwenda kulala itasaidia kunyevua midomo yako.ukifanya hivi kwa muda mrefu, itakusaidia kuongeza ulaini wa midomo yako na kuifanya kuwa na muonekano wa kuvutia sana.

Tumia Lip Balms zinazosaidia Kukulinda kutokana na athari za miale ya jua.

Jua kali ni 'adui wa ngozi yako'; na hapa najumuisha ngozi ya midomo yako pia. Ili kuzuia athari ya jua kwenye lips zako, tumia bidhaa zenye SPF 15 (Sun Protection Factor).

Tumia mchanganyo wa asali na sukari

Tengeneza mchanganyo wa asali na sukari, kisha paka kwenye lips zako kwa dakika kadhaa. Hii itasaidia kuiweka ngozi ya midomo yako ikiwa nyororo na laini. Pia husaidia kuondoa seli za ngozi zilizokufa.

Tumia vyakula vya kujenga mwili

Ili 'upate' lips laini na za kuvutia ni muhimu sana kupata vyakula vya kujenga mwili, vyakula kama samaki, mayai, nyama, mboga za majani na matunda ni muhimu sana kwa afya ya ngozi yako kwani vina vitamini B na C ambazo ni muhimu kwa afya ya ngozi yako. Pia samaki ni muhimu sana kwani ina omega-3 fatty acids ambayo ni muhimu kwa ajili ya kusawazisha ngozi yako.