http://www.swahilihub.com/image/view/-/4710658/medRes/2077958/-/elj9vvz/-/mikono.jpg

 

Jinsi ya kutunza mikono kuzuia ukavu

Mikono

Mikono iliyo na ukavu. Picha/MTANDAO 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Monday, August 13  2018 at  10:57

Kwa Muhtasari

Ni vigumu sana kupata moisturiser ambayo haina madhara kwa ngozi yako na inayoweza kusaidia ngozi iwe laini.

 

HALI ya ukavu wa mikono inaweza kusababishwa na vitu vingi hasa baridi au kutopaka ‘moisturiser’.

Hali hii inaweza kuwa mbaya zaidi na kusababisha kukauka.

Ni vigumu sana kupata moisturiser ambayo haina madhara kwa ngozi yako na inayoweza kusaidia ngozi iwe laini.

Iwapo kwako hali ni kama hiyo, huhitaji kuwa na wasiwasi kwani si lazima utumie hela nyingi kununua mafuta ambayo yatamaliza tatizo hilo.

Unaweza pia kutumia njia za kiasili kama ifuatavyo:

Tengeneza mkorogo mzito kwa kutumia parachichi nusu, mafuta ya mizeituni kijiko kimoja na apple cider vinegar kijiko kimoja. Changanya vizuri kisha paka kwenye mikono yako na ukae nayo kwa dakika 15, nawa kwa maji ya fufutende. Utaona mikono imekuwa laini; fanya hivi kila siku ili upate matokeo mazuri.

Chukua apple cider vinegar changanya na maji kwenye bakuli, kisha loweka mikono yako humo kwa muda. Toa na uache mikono ikauke yenyewe. Apple cider vinegar inasaidia kuondoa maumivu kutokana na mikono kukauka sana.

Chukua kiini cha yai, juisi ya ndimu na mafuta ya mizeituni kijiko kimoja. Changaya vizuri katika bakuli kisha paka kwenye mikono yako na kaa nayo kwa dakika 15. Nawa mikono na maji ya fufutende kisha paka losheni.

Pamoja na kukabiliana na tatizo hili, maji pia yana umuhimu katika mwili wa binadamu. Katika hali ya kawaida, upungufu wa maji unaweza kuchangia kukauka kwa mikono. Ni vyema mtu kunywa angalau glasi nane za maji kila siku ili kusaidia kulainisha ngozi mbali na umuhimu mwingine mwilini.

Matunda yenye majimaji kama karoti, matango, nyanya na tikitimaji yanaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na tatizo hili. Zoea kula mboga za majani kwa sababu hizi huwa na muhimu wake pia.