http://www.swahilihub.com/image/view/-/4802712/medRes/2142251/-/geyru4z/-/fau.jpg

 

Serikali yatoa maagizao kuhusa dawa

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile  

Na Kalunde Jamal

Imepakiwa - Friday, October 12  2018 at  15:41

Kwa Muhtasari

Ubora wa dawa Tanzania ni mzuri wenye viwango vya hali ya juu

 

 

Dar es Salaam. Serikali imekemea dhana potofu kuwa dawa za kutoka nchi fulani ni bora kuliko nyingine.

Pia imepiga marufuku madaktari nchini kuwaandikia wagonjwa majina ya biashara ya dawa, badala yake kuandika majina ya asili na kazi ya kutafsiri kuwaachia wafamasia.

Aidha, imewataka wadau wa afya kuoanisha na kuhuisha mifumo yao ya kielektroniki ili waweze kushirikiana na kutoa takwimu sahihi za dawa.

Maagizo hayo yalitolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile wakati akifungua mkutano wa wadau wa ugavi wa dawa katika kuangalia mfumo mzima wa upatikanaji wake, vifaatiba na vitendanishi.

Dk Ndugulile alisema ubora wa dawa Tanzania ni mzuri wenye viwango vya hali ya juu na ni sawa na zinazotumika maeneo yoyote duniani.

Naye Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia afya, Dk Zainab Chaula alisema wadau wa afya ambao hawatajitambulisha serikalini hawataruhusiwa kufanya shughuli zao nchini.

Alisema wapo wadau 8,700 lakini haijulikani wanafanya nini na wapo wapi hivyo wanatakiwa kujitokeza na kubainisha shughuli zao waweze kutambulika rasmi.