Shilole awafunda wanaokimbilia ndoa

Imepakiwa - Wednesday, May 15  2019 at  13:26

 

Mwanamuziki Zuwena Mohamed maarufu Shilole amesema ni vyema wapenzi wakajuana kabla ya kuingia kwenye ndoa ili nyumba iwe na maelewano.

Alisema si vyema kufunga ndoa kwa sababu yoyote ile isipokuwa mapenzi ya dhati kwani ndiyo yanayoweza kumfanya mtu amvumilie mwenziwe.

“Kwa mfano mtu anafunga ndoa kwa sababu ya Mwezi wa Ramadhan, hii sawa na ni kumdanganya hata aliyetuumba kwa kuwa inaweza kuvunjika ikikosa masikilizano,” alisema.

“Kama wewe ni mfuasi mzuri wa dini huwezi kukurupushwa na nyakati, wakati wote unapaswa kutenda mema ikiwamo kuacha zinaa,” alifafanua.

Shilole ambaye pia ni mmiliki wa mgahawa wa Shishi Food alisema wapendao wafunge ndoa kwa kuwa ni jambo linalomfurahisha Mungu lakini waongozwe na mapenzi na maelewano.