http://www.swahilihub.com/image/view/-/4391518/medRes/1937695/-/1544qrq/-/area.jpg

 

Sokoine aenziwe kwa kuwajali wakulima nchini Tanzania

Edward Muringe Sokoine

Marehemu Edward Muringe Sokoine aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Picha/MAKTABA 

Na MHARIRI – MWANANCHI

Imepakiwa - Monday, April 16  2018 at  06:11

Kwa Muhtasari

Marehemu Waziri Mkuu Edward Sokoine aliamini kuwa siasa ni kilimo ndiyo maana siku zote alipigania sekta hiyo kwa kauli na vitendo.

 

JUZI Aprili 12, 2018, ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka 34 tangu Waziri Mkuu Edward Sokoine aage dunia kwa ajali ya gari wakati akitokea Dodoma baada ya kumalizika kikao cha Bunge alichokuwa akihudhuria.

Yako mengi ya kukumbukwa kuhusu utendaji wa kizalendo aliokuwa nao Sokoine aliyefariki dunia mwaka 1984 akiwa na umri mdogo wa miaka 45 lakini kubwa ni jinsi alivyotilia mkazo kilimo.

Sokoine aliamini kuwa siasa ni kilimo ndiyo maana siku zote alipigania sekta hiyo kwa kauli na viitendo.

Kiongoozi huyo alikuwa mchapakazi na ndoto yake ilikuwa ni kutaka Tanzania ijitosheleze kwa chakula na ziada iuzwe nje ya nchi. Alitaka pia izalishe izalishe kwa wini mazao ya biashara kama pamba, kahawa, chai, monge na kakao kwa lengo la kuliingiizia fedha za kigeni.

Sokoine alifanya hivyo akiamani kuwa kilimo ndio uti wa mgango wa uchumi wetu.

Hakutaka Taifa liwe ombaomba ila lenye nguvu kiuchumi

Ndiyo maana alijitahidikuliweka msingi mzuri wa maendeleo kupitia elimu ya kijitegemea na siyo kutafuta kazi za kuajiriwa.

Hata hotuba yake ya mwisho kwa Taifa aliyoitoa siku moja kabla ya kifo hake wakati alipokuwa akiahirisha kikao cha Bunge mjini Dodoma Aprili 11 1984 alisema ni heri mkulima atakayekamatwa akiiba mbolea ili aitumie vizuri kwenye shamba lake.Hio tutamsamehe laiki ole wake kiongozi atakayekamatwa kwa kufanya ubadhirifu wa mali ya umma.

Kutokana na kuipa umuhimu mkubwa kilimo,Sokoine ndiye kiongozi wa kwanza mabwana na mabibi kilimo na mifugo wakaishi vijijini kariu na wananchi . Kwa msngi hiyo alifanya Tanzania isimame vyemakatika dhana ya kilimo kama uti wa mgongo  wa Taifa.

Wakati tukiadhimisa miaka 34 ya kifo cha Sokoinebado mjadala naendela kufanywakutoka kwa watu mbalimbali wakilalamika kuwa kilimo kimesauliwa na asilimia kubwa ya wakulima wanaendela kutumia zana duni za kilimo . Wataalamu wanalalamikiwa kutofika vijijini na baadhi yaowameelezwa kuamua kukimbilia kwenye siasa kutafuta maslahi mazuri zadi.

Kwa hiyo, ipo haja kwa Serikali kufanya mapinduzi ya kilimo ambayo yatakwenda sambamba na mkakati wa Tanzania Tanzani ya viwanda  kwa kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya kuwavutia watu wengi   kungia katika sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo maalumu ya kuendeshea shughuli  za kilimo, biiashara na kupeleka miundombinu yote muhimu.

Jambo lililo wazi ni kwamba waklima wana matatizo mengi ya uhaba wa wataalamu, uhhaba wa masoko ya mazao yaona hasa suala la bei ndgo ya mazao.

Wapo wafanyabiashara wanaokwenda kununua mazao kwa wakulima kwa hila kama vile matumizi ya ‘lumbesa’ na kununua mazoa yao yakiwa shambani bbadaya ya sokoni.

Rai yetu kwa viongozi wa Serikali, watunga sera na wanasiasa tumuenzi hayati Sokoine kwa kutatua kero za wakulima ili waweze kulima kitaalamu na kwa faida.

Kwa kuwa tunaamini kuwa kilimo ni uhai, basi tukifanye kiwe sehemu ya maisha yetu.

Tahariri ya Mwananchi,

Mwananchi Communications Limited (MCL)

S.L.P. 19754 Dar es Salaam-Tanzania

SIMU +255222450875 au +255754780647