http://www.swahilihub.com/image/view/-/2510316/medRes/867403/-/s10inc/-/WILLYYY.jpg

 

Take Dasiva da rapper adai aliwahi vuta bangi na Willy Paul

Willy Paul

Willy Paul akiwatumbuiza mashabiki awali. Picha/MAKTABA 

Na THOMAS MATIKO

Imepakiwa - Sunday, March 19  2017 at  21:12

Kwa Mukhtasari

Mmoja wa wasanii kwenye kambi ya rapa wa kike maarufu ambaye inadaiwa ni msagaji, Noti Flow, kadai eti yeye na staa mtatanishi wa injili, Willy Paul walikuwa ni washikaji wakubwa zamani na mara nyingi walikuwa wakivuta bangi pamoja.

 

MMOJA wa wasanii kwenye kambi ya rapa wa kike maarufu ambaye inadaiwa ni msagaji, Noti Flow, kadai eti yeye na staa mtatanishi wa injili, Willy Paul walikuwa ni washikaji wakubwa zamani na mara nyingi walikuwa wakivuta bangi pamoja.

Take Dasiva da rapper, aliyeshirikishwa na Noti Flow kwenye kazi yake mpya ‘Drink & Party’ kadai kuwa yeye na Willy Paul walikuwa washikaji sana enzi za udogo wao kwa sababu waliishi mtaa mmoja na mara kadhaa wangetangamana vijiweni na kuchemsha bongo kwa ku-puff  bangi

“Hiyo ilikuwa ni zamani kidogo kabla hajakuwa staa, tulikuwa tunaishi mtaa mmoja na tungetangamana sana hivyo kwetu kuvuta banhi na mshikaji Willy Paul ilikuwa jambo la kawaida sana,” amedai Take Dasiva da rapper.

Kauli ya rapa huyo chipukizi imechukuliwa na baadhi ya mashabiki kuwa kama kiki vile na kaitoa kipindi Willy Paul akiwa Tanzania kwa kile kinachoonekana kuwa jitihada zake za kutaka kufanya kolabo na staa ambaye yeye humhusudu sana, Diamond Platnumz.