Tutilie mkazo elimu ya matumizi ya reli

Imepakiwa - Monday, March 18  2019 at  09:31

 Usafiri wa reli ni moja ya huduma muhimu na inayogusa kundi kubwa la watu katika Taifa lolote ulimwenguni.

Kwa Tanzania, huduma hii iliyokuwa tegemeo miaka ya nyuma, ilidorora katika baadhi ya maeneo kabla ya Serikali kuanza kuweka mkakati mahsusi wa kuifufua.

Ukiondoa utekelezaji wa mradi wa reli ya kisasa (SGR) unaoendelea kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro kwa awamu ya kwanza na Morogoro kwenda Makutopora katika awamu ya pili, tumeshuhudia ukarabati wa reli inayotumika sasa hatua ambazo tunaamini zinalenga kumsaidia mwananchi wa kipato cha chini kwa njia mbalimbali.

Njia hizo ni pamoja na kuwa na uhakika wa usafiri kwa gharama nafuu na kusafirisha bidhaa kwa bei ndogo hivyo kupunguza makali ya maisha.

Akizindua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa Aprili 2017, Rais John Magufuli alitaja baadhi ya faida zake kuwa ni pamoja na kutoa ajira kwa watu takriban milioni moja, kusaidia kutunza barabara ambazo zinaharibika kwa sababu ya kusafirisha mizigo mikubwa na nafasi ya reli hiyo katika kukukuza sekta nyingine nchini akieleza kwamba malighafi mbalimbali zitasafirishwa kwenda kwenye maeneo ya viwanda.

Hatua hiyo ya kimaendeleo katika sekta ya usafiri na usafirishaji ina changamoto zake, mojawapo ni matumizi sahihi ya njia za reli kwa wananchi na vyombo vingine.

Pengine kutokana huduma hiyo kutokuwa pana, baadhi ya watumiaji wa reli ama hawajui au hawachukui hatua za tahadhari wanapokuwa katika maeneo ya miundombinu hiyo.

Pia, watoa huduma hiyo nao hawajatoa elimu ya kutosha kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya reli, wanaoendesha vyombo vingine vya moto na baiskeli juu ya sheria na hatua za kiusalama wanazotakiwa kuchukua wawapo katika njia ya treni au karibu yake.

Matukio ya ajali kama hii iliyotokea juzi jijini Tanga ambayo ilisababisha kifo cha mtu mmoja papo hapo na wengine 30 kujeruhiwa baada ya basi dogo aina ya Toyota Coaster kugonga treni, inapaswa kutuzindua na kila mmoja kwa nafasi yake achukue hatua kuhakikisha kwamba hili halijirudii tena.

Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16, kifungu cha 224, inabainisha makosa na adhabu kwa mtu yeyote ambaye, anakusudia kumjeruhi au kuhatarisha usalama wa mtu yeyote anayesafiri kwa njia ya reli yoyote iwe ni mtu mahsusi au la.

Kifungu hicho pia kinabainisha kuwa mtu ambaye, bila ya halali, lakini bila kusudio lililoelezwa na kifungu cha (1) anasababisha usalama wa mtu yeyote anayesafiri kwa reli kuwa hatarini atakuwa anatenda kosa.

Kama tulivyoeleza awali, hivi sasa kasi ya uimarishaji wa huduma ya reli inaongezeka, kwa maana hiyo watumiaji na watakaohusika kwa njia moja au nyingine na miundombinu yake nao pia wanaongezeka.

Hivyo basi, ni wajibu wa kila mdau kwa nafasi yake kuhakikisha sheria zote zinazohusiana na matumizi ya reli na miundombinu yake zinafikishwa sasa kwa wananchi sambamba na zile za usalama barabarani.

Itakuwa jambo jema huduma za reli hasa ile ya kisasa zitakapoanza kuwakuta wananchi wakiwa tayari na uelewa mpana wa sheria, taratibu na wajibu wao katika kulinda rasilimali hiyo muhimu kwa uchumi.

Kwa sababu hiyo, ipo haja kuanzia sasa kila anayehusika na miundombinu ya reli kutoa elimu ya matumizi na sheria zinazohusiana na sekta hiyo ya usafiri na usafirishaji kwa wadau wake ili kuepusha vifo kutokana na ajali au uzembe mwingine wowote na hujuma.

Treni ndio usafiri unaobeba abiria wengi zaidi kwa pamoja kama ilivyo pia katika mizigo. Tunataka kuona elimu ikitolewa kwa njia mbalimbali zikiwamo za vipeperushi, vyombo vya habari, matamasha na nyinginezo ilimradi kila mtu awe mlinzi wa miundombinu hii muhimu kwa manufaa yake na Taifa.

mwanzo| Habari|

mwanzo| Habari| Jifunze Kiswahili| Blogu Na Ukumbi| MAKTABANI JISOMEE| picha| video| Makala|