http://www.swahilihub.com/image/view/-/5057842/medRes/2303276/-/g57uk4/-/matunda+pic.jpg

 

Umuhimu wa kula matunda

Na Mwandishi wetu

Imepakiwa - Friday, April 5  2019 at  10:37

 

Je, ulaji sahihi ni upi unaokupatia virutubishi vingi kati ya kula tunda zima au kunywa juisi ya matunda?

Mtaalamu huyo anashauri kula tunda kama tunda ili kupata virutubishi vyote katika tunda. Pia, unywaji wa juisi ya matunda pia ni bora iwapo haitaongezwa kitu cha kuhifadhi ili kukaa kwa muda mrefu ubora wake utafanana na kula tunda zima.

“Juisi ya kutengeneza nyumbani inakuwa na nyuzinyuzi kwa wingi kama ilivyo katika tunda, huku juisi zinazonunuliwa madukani hazina viwango na ubora kama juisi za kutengenezwa nyumbani kutokana na kuongezwa vihifadhi na ladha,”anasema.

Anafafanua kuwa wakati wa utengenezaji wa juisi nyumbani hakikisha unaweka na sehemu ya maganda ya tunda inayoliwa ili kuboresha virutubishi.

Hata hivyo, mtu anashauriwa kula matunda yaliyo katika msimu ulipo ili kupata matunda yaliyo fresh (halisi).

Lyimo anatoa tahadhari kuwa juisi za madukani ikiwa zitatumiwa kwa muda mrefu humuweka mtumiaji katika hatari yakuongezeka uzito.