Usafiri mwendokasi usiwe kero kwa wananchi

Imepakiwa - Friday, March 15  2019 at  10:43

Wakazi wa Kimara na maeneo mengine ya pembezoni mwa jiji wanaotumia barabara ya Morogoro wanalia kilio ambacho sisi tunadhani kimekosa msikilizaji.

Aghalabu, kumekuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa mabasi katika vituo hasa wakati wa asubuhi watu wanapokwenda kazini na jioni wanaporejea makwao. Mabasi hayatoshelezi mahitaji ya abiria. Kinachotokea ni vurugu na sintofahamu za mara kwa mara kati ya abiria na wahusika vituoni, kama tulivyoripoti jana baada ya abiria katika eneo la Kimara kumlazimisha dereva wa basi moja kuwapakia.

Wakati abiria wakichoshwa na ugumu wa usafiri, dereva wa basi hilo alitaka kutoka kituoni bila ya abiria ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa mabasi ya Udart kutopakia abiria katika eneo ambalo basi halijapangiwa njia.

Hii sio mara ya kwanza kwa usafiri huo ambao kimsingi ulitarajiwa kuwa kimbilio na nusura kwa wananchi, kudorora na kuzusha sintofahamu na vurugu kwa watumiaji wake. Sasa si ajabu kusikia huduma hiyo ikilalamikiwa kufanya kazi kwa kusuasua.

Ni mpaka lini hali hii itaachwa iendelee? Tufike mahala mamlaka husika zirejee misingi ya kuanzishwa kwa huduma hii na kuiboresha ili iwavutie watumiaji zaidi, badala ya kero zilizopo sasa kiasi cha abiria kutamani kurudi kwenye daladala.

Tunadhani huu ni wakati mwafaka kwa Serikali kuingilia kati kuhakikisha huduma hii inarudi katika ubora wake kama ilivyokuwa awali.

Wakazi wa Dar es Salaam wanataka kuona mradi kunafanyia kazi changamoto zilizopo zikiwamo za uhaba wa mabasi, malipo ya tiketi na uchukuaji wa abiria vituoni.

Ikibidi, wakati mamlaka zikijipanga kuupa sura ya faraja mradi huu, Serikali iruhusu daladala kuendelea kufanya kazi japo kwa muda katika maeneo yote ya mradi ambayo wananchi wanatatizika kwa kukosa usafiri, hivyo kuathiri shughuli nyingi za maendeleo ya Taifa.

Huu ni mradi muhimu na wa kipekee kwa Taifa, tuujali na tuupe hadhi stahiki ili uvutie wengi zaidi badala ya kuwa kero.

Miaka kadhaa iliyopita Serikali ilianza ujenzi wa miundombinu ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka katika Jiji la Dar es Salaam (Dart).

Mwaka 2017, Rais John Magufuli akazindua mradi huo ikiwa ni awamu ya kwanza yenye urefu wa kilomita 20.9 kutoka Kimara hadi Kivukoni.

Tunatambua kuwa mpango huu unaendeshwa kwa awamu na tayari mipango imeshaanza ya ujenzi wa miundombinu katika maeneo mengine ikiwamo ile inayotarajiwa kupita katika barabara za Kilwa, Kawawa, Sokoine, Bandarini, Gerezani na Chang’ombe.

Mradi huu wa mabasi yaendayo haraka pamoja na mambo mengine, unalenga kuondoa msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam na hivyo kutoa nafuu ya usafiri kwa wakazi wa wanaoongezeka kila mwaka.

Ni mpango ambao kuja kwake kuliwakosha wengi na kuwapa kicheko, lakini kadri siku zinavyosonga huduma hiyo imegeuka kuwa shubiri na kero kubwa kwa wakazi ambao wanautegemea.

Kibaya zaidi ni pale wakazi wa jiji hilo wanapohisi kuwa hakuna jitihada za dhati za kuwaondoshea masaibu ya usafiri wanayokumbana nayo hivi sasa.