Ushindi wa Mwakinyo uwe darasa kwa wadau

Imepakiwa - Monday, March 25  2019 at  14:18

 

Tanzania imeendelea kuwika kwe-nye ulimwengu wa mchezo wa masumbwi baada ya bondia wake, Hassan Mwakinyo kumtwanga Sergio Gon-zalez wa Argentina katika pambano lisilo la ubingwa.

Pambano hilo lililofanyika juzi usiku kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Miku-tano wa Kenyatta (KICC), Nairobi, Kenya lilikuwa kali kwa pande zote mbili tangu raundi ya kwanza.Kwa muda sasa, Mwakinyo alikuwa kwe-nye mazoezi makali nchini England chini ya kocha wake, Tony Bellew.

Pamoja na kwamba pambano halikuwa la ubingwa, lakini tunampongeza kutokana na mafanikio ambayo amekuwa akiyapata nchi ya ardhi ya nyumbani hivyo kulitan-gaza vyema jina la Tanzania katika medani za mchezo huo.

Hii ni mara ya pili katika siku za karibuni kwa bondia huyo mkazi wa Tanga kuibu-ka na ushindi katika mapambano yake ya kimataifa.Septemba mwaka jana, alitawala vichwa vya habari na mitandao ya kijamii baada ya kumshinda bondia wa Uingereza, Sam Eggington.

Katika pambano hilo, mwamuzi alilazimika kumwokoa Muingereza huyo.Tangu wakati huo, Mwakinyo amekuwa maarufu ndani na nje ya nchi kiasi cha kuibua upya hamasa ya mchezo huo kwa vijana iliyokuwapo wakati familia ya kina Matumla ikiongozwa na Rashid ilipokuwa ikitamba na baadaye Francis Cheka.

Tunaamini kwamba kufanya vizuri kwa Mwakinyo katika michezo yake hiyo miwili ni mwanzo mzuri kwake wa kupanda kati-ka chati za mchezo huo lakini pia, kuwa-hamasisha vijana wengine wanaoupenda.

Hamasa tunayoizungumzia hapa ina mambo mawili; mosi, kwamba wakitia nia ya dhati na kuwa na nidhamu ya mchezo, wanaweza kuwa kama yeye au hata kum-zidi.

Pili, wanaweza kujitengenezea maisha yao na jamii inayowazunguka. Hivi sasa Mwakinyo anadhaminiwa na SportPesa na kwa ushindi wake huo, ni dhahiri kwamba hawezi kukaa muda mrefu bila ya kupata mchezo, yote hayo yakimaanisha kuingiza kipato.

Ikumbukwe kwamba katika masumbwi, kadri bondia anavyopanda chati, ndivyo dau lake pia linavyopanda sambamba na kupata wadhamini na kutangaza bidhaa na huduma mbalimbali ambayo yote ni mapato makubwa.Tunaamini katika siku zijazo, Mwakinyo atakuwa balozi mzuri wa mchezo huo iki-wa ni pamoja na kuiletea heshima Tanza-nia kwa kuzoa mikanda ya kimataifa.

Pamoja na imani hiyo tuliyonayo kwa Mwakinyo, tunaiomba Serikali, wadau wa michezo na zaidi huu wa masumbwi kuhakikisha kwamba kijana huyu anaan-daliwa kuwa bondia wa viwango vya mikanda mikubwa zaidi dunia.

Wapo wanaoweza kutoa ushauri wa kitaalamu, wengine wanaweza kumjengea mazingira mazuri ya kujiandaa na hata hamasa alimradi ajihisi kwamba jukumu la kushinda kwake katika mchezo ulio mbele yake ni la lazima kwani kila Mtanzania yupo nyuma yake.

Aidha, ushindi huo unapaswa kuwa darasa kwa vyama vya ngumi na Seri-kali la kuanza kuwasaka kina Mwakinyo wengine kwani tunaamini kwamba wapo wengi lakini hawajulikani na wao pengine hawapati nafasi ya kuonyesha uwezo wao.