Usimdharau usiomjua

Na  Yahya O.Barshid (YOB)

Imepakiwa - Wednesday, April 10  2019 at  11:33

 

Waswahili wamesema, kiburi si maungwana,

Kiburi si kitu chema, kisha hakileti maana,

Humpa mtu kilema, cha mwendo wakujiona,

Dharau si maungwana.

 

Kiumbe acha jeuri, huko ni kujisahau

Ishi na watu vizuri, usiwe mwenye dharau,

Onyesha tabia nzuri, hiyo ndiyo zambarau,

Dharay si maugwana.

 

Mpanda ngazi hushuka, daima juu hukai,

Maisha hubadilika, ujuae hashangai,

Usije weka tabaka, hali bado uko hai,

Dharau si maungwana.

 

Kwa hiyo hapa tamati, nimefikia mwishoni,

Usomjua kwa dhati, hilo angalia sana,

Hutoipata sirati, iendayo kwa Rabana,

Dharau si maungwana.

Mwisho.