Victoria Kimani azindua video ya March Along

Victoria Kimani

Mwanamuziki maarufu Kenya, Victoria Kimani. Picha/THOMAS MATIKO 

Na PAULINE ONGAJI

Imepakiwa - Saturday, July 15   2017 at  13:40

Kwa Mukhtasari

Victoria Kimani amezindua video ya kibao chake March Along iliyokuwa imesubiriwa.

 

HATIMAYE mwanamuziki Victoria Kimani amezindua video ya kibao chake March Along iliyokuwa imesubiriwa.

March Along ni video ya sita ya msanii huyu kutoka kwaa albamu yake ya kwanza SAFARI.

Kibao hiki ni kwa heshima ya wanawake barubaru wanaojikakamua kufanikiwa maishani licha ya changamoto wanazokumbana nazo kila siku.

Video hiyo imefanikishwa kwa ushirikiano wa Joe x / UJ pro na Iju ishaga.