Vigezo bora chama cha siasa

Imepakiwa - Wednesday, April 3  2019 at  09:15

 

Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa imetaja vigezo vitatu vinavyobainisha ubora wa chama cha siasa nchini, ikiwamo uimara wa kitaasisi katika maeneo mbalimbali.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya siasa, Sisty Nyahoza amesema kuna baadhi ya vyama visivyokuwa hata na sera zinazoonyesha itikadi yake kimaandishi ambayo ofisi hiyo itaanza kuvibana.

“Kuna vyama document yao tu ya sera, siyo kuisema kichwani, utazipata? Tunaanzia hapo(kwenye sera), subiri utaona marekebisho ya sheria inavyokwenda, tunataka exactly kwanza tujue sera, Imani yake ni ipi in document(kimaandishi) ili mtu akija tumwambie Imani ya chama hiki ni hii hapa,”alisema siku chache zilizopita wakati wa mahojiano na gazeti hili.

Kwa mujibu wa ofisi hiyo, ofisi hiyo hadi kufikia Novemba 2016, idadi ya vyama vya siasa vilivyosajiliwa kisheria vilikuwa ni 19 baada ya kufutwa vyama vitatu Chausta, APPT-Maendeleo na Jahazi Asilia.

Nyahoza alisema vigezo vingine ni ukomavu wa Demokrasia ndani ya chama na utii wa Sheria zilizopo ikiwamo Sheria ya Vyama vya siasa ya 1992, marekebisho ya 2018.

“Tunapima kwa kuangalia utekelezaji wa sheria na misingi ya demokrasi ndani ya vyama,tunapima institutionalism, kwa manaa ya kuendesha vipi chama kama taasisi, pia tunatumia ripoti za CAG zinazotoka kuangalia utaasisi katika mifumo wa kifedha,” alisema.

huku akisisitiza taasisi imara haiwezi kuyumba kwa mwanachama mmoja kuondoka ndani ya chama husika.

Msingi wa mahojiano hayo ni baada ya Nyahoza kutoa nafasi ya mahojiano ya kina kwa mwandishi aliyehitaji kauli kutoka ofisi hiyo mlezi wa vyama kuhusu madai ya wafuasi wa Cuf kutaka kuvamia mkutano wa ACT Machi 27, ukumbi wa PR uliopo Temeke jijini Dar es Salaam.