Wananchi, polisi wazuie utekaji wa watoto

Na GAZETI LA MWANANCHI

Imepakiwa - Thursday, September 7  2017 at  15:30

Kwa Mukhtasari

TANGU wiki iliyopita, gazeti hili lilikuwa na mwendelezo wa habari za tukio la kusikitisha lautekaji wa watoto wawili Moureen David miaka 6 na Ikram Salim wa miaka 3 ambao juzi wamepatikana wakiwa wameuawa

 

Watoto hao ambao ni wakazi wa kata ya Olasiti, Arusha walitekwa siku tofauti. Wakati Moureen alitekwa Agosti21 jioni, Ikram alitekwa Agosti 26 saa 12.00 jioni . Juzi miili yao ilipatikana katika shimo la majitaka eno la Mji Mpya Mtaa wa Olkerian

Kinachosikitisha zaidi ni kauli ya Kassim Salum mzazi wa Ikram kwamba siku ya tukio alitoa taarifa kwa polisi lakini haikufika. Kwa hali hiyo, yeye peke yake hakuweza kukabiliana na wahalifu hao.

Kimsingi si hoja yetu kuelekeza hoja yetu  kwa yeyote, bali  tunachosema ni kwamba ushirikiano kati ya wananchi na polisi ni muhimu kkatika kukabiliana na uhalifu.

Pia ni mhimu kuaminiana. Inawezekana mtu akatoa taarifa kuhusu tukio la uhalifu lakini polisi wakachululia kama kama mzaha na kuhelewa kifika eneo waliloitwa au kutofika kabisa.

Tunajua polisi wamewezeshwa kwa upewa nyennzo nyingi ili kuwaezsha kufanya kkazi kwa urahisi uanzia ngazi ya wilaya hadi mkoani Pia wana usafiri wa kuenya vichochoroni ambao ni pikipiki.

Kinachohitajika hapa ni ni kutekeleza majukumu yaokwa muibu wa sheria ya kuunda jeshi hilo. Hofu yetu ni kwamba polisi wataanza kufanya kazi zao kwa kwastaili hiyo kwa baadhi ya matukio. Hii ni hatari kwa sababu wahalufi hawapigi hodi.

Matukio ya utekaji watoto tumewahi kusikia yakitokea nje ya nchi na wahalifu hao wakiwatumia watoto wakidai malipo ya kukomboa mateka, lakini watekaji wengine hasa waasi au magaidi hutumia watoto kama ngao yao ya kuepuka kushambuliwa au kukamatwa.

Kuna msemo wa wahenga ambao unasema ‘tahadhari kabla ya hatari”. Hivyo ni vyema kwa jeshi letu kuchukua tahadhari. 

Lakini pia wananchi nao ni wadau wakubwa wa kulisaidia jeshi la polisi ili waweze kufanya kazi zao kwa weledi na kwa wakati mwafaka.

Wahalifu tunaishi nao mitaani, wengine ni ndugu zetu. Hakuna maana kama suala la utekaji la watoto wakaachiwa polisi pekee wakati wananchi wana taarifa zote kuhusu watu hao

Tunaamini kilichotokea Arusha kitatufumbua macho sisi sote kuona umuhimu wa kushirikiana na vyombo vya habari kukabiliana na uhalifu nchini.

Ushauri wtu kwa wananchi  ni kwamba wawe tayari kudumisha ushirikiano kati yao na jeshi la polisi watoe taarifa kwa kwa mamlaka husika  pale wanapoona tukio lisilo la kawaida  katika eneo la makazi yao au mmaeneo yao ya uzalishaji mali.

Jeshi la polisi limesambaza namba za bure  za kutoa taarifa za uhalifu wowote lakini siku hizi makamanda wa polisi wa mkioa na wilaya wameanzisha utamaduni wa kutoa wa kutoa namba zao  za mkononi wanazotumia kwenye kazi.

Tunawashauri wananchi wazitumie namba hizo kudumisha usalama na Amani kila siku. Ni vyema kila mmoja wetu akawa mlinzi wa watoto hawa wa maana linalomkuta mmoja wao linaweza kumkuta mwingine.

Pia tunavishauri vyombo vya dola kuzifanyia kazi kwa haraka na kutunza utambulisho wa wato taarifa illi vitendo hivi kabla havijashamiri katika maeneo mengi  ya nchi.

Tukishirikiana tunaweza udumisha Amani yetu.